Maprofesa wa Iran wataka kuhitimishwa jinai za utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70590-maprofesa_wa_iran_wataka_kuhitimishwa_jinai_za_utawala_wa_kizayuni
Maprofesa wa Vyuo Vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametoa mwito wa kuhitimishwa mara moja jinai zote zinazofanywa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni dhidi wananchi madhulumu wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 26, 2021 23:07 UTC
  • Maprofesa wa Iran wataka kuhitimishwa jinai za utawala wa Kizayuni

Maprofesa wa Vyuo Vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametoa mwito wa kuhitimishwa mara moja jinai zote zinazofanywa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni dhidi wananchi madhulumu wa Palestina.

Katika barua yao kwa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Maprofesa na wasomi mashuhuri wapatao 160 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametaka kukomeshwa jinai za kivita na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Wamelaani mauaji ya halaiki ya hivi karibuni dhidi ya Wapalestina wa Gaza hususan wanawake, watoto wadogo na wanafunzi wa shule za sekondari ya Vyuo Vikuu.

Wapalestina 248 waliuawa shahidi na maelfu ya wengine walijeruhiwa katika mashambulizi ya siku 12 ya Wazayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza. 69 kati ya waliouliwa shahidi walikuwa watoto wadogo, 39 wanawake na wazee wakongwe 17.

Sehemu moja ya barua hiyo ya Maprofesa wa Vyuo Vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema: Katika mashambulio hayo, idadi kubwa ya wanawawake wa Kipalestina, watoto wadogo, wanafunzi wa shule za upili na wanachuo waliuawa shahidi katika wimbi kubwa la mashambulio huko Gaza kwa kutumia silaha nzito za kisasa.

Ukatili wa askari wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza

Katika barua hiyo, Maprofesa na wanaakademia wa Iran wamemhtubu Katibu Mkuu wa UN kwa kumuambia kuwa: Kwa kuzingatia kuwa vitendo hivi ni mifano hai ya mauaji ya kimbari na jinai za kivita, Vyuo Vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu vinataraji utachukua hatua za kuzuia kujiriri kwa jinai hizo, kwa mujibu wa malengo na majukumu ya Umoja wa Mataifa.

Kadhalika wametaka kupandishwa kizimbani wahusika wote wa jinai hizo katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa kutumia miongozo na michakato ya UN na Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo.