Kamanda wa IRGC: Iran imesimama kidete kukabiliana na Marekani na waitifaki wake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i79976-kamanda_wa_irgc_iran_imesimama_kidete_kukabiliana_na_marekani_na_waitifaki_wake
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema katika kipindi cha miaka 43 iliyopita, Iran imesimama kwa adhama katika kukabiliana na mashinikzo ya juu kabisa ya Marekani na waitifaki wake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2022 08:21 UTC
  • Kamanda wa IRGC: Iran imesimama kidete kukabiliana na Marekani na waitifaki wake

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema katika kipindi cha miaka 43 iliyopita, Iran imesimama kwa adhama katika kukabiliana na mashinikzo ya juu kabisa ya Marekani na waitifaki wake.

Meja Jenerali Hossein Salami Kamanda Mkuu wa IRGC ameyasema hayo huko Golpeygan katika kikao cha kuwakumbuka mashahidi na kuongeza kuwa: "Leo mfumo mtakatifu wa Kiislamu wa Iran unatajwa kwa fahari na heshima duniani kote."

Meja Jenerali Salami ameendelea kusema kuwa, si kazi rahisi kusambaratisha mfumo wa kibeberu wa Marekani ambao katika historia yake umepelekea kusambaratika mifumo mingine duniani na kuongeza kuwa, kufanikiwa kusambaratisha sera za kimataifa za Marekani tena jambo lenyewe lifanikishwe na nchi ambayo imewekewa vikwazo ni jambo ambalo limewezekana tu kwa irada na uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Majaribio ya makombora ya Iran

Kamanda Mkuu wa IRGC hali kadhalika amesema leo wananchi wa Iran wanajitokeza katika medani wakiwa na ufahamu kamili huku mfumo wa Kiislamu ukiwa uko imara kabisa. Ameendelea kusema kuwa iwapo mfumo wa Kiislamu wa Iran haungekuwa na nguvu na uwezo basi maadui wangekuwa wameshaivamia nchi hii lakini leo maadui wameshindwa kusonga mbele na wanakiri wazi kuhusu unguvu na uwezo mkubwa wa Iran.