Rais Raisi: Ahul Bayt AS ni siri ya Umoja wa Kiislamu
(last modified Thu, 01 Sep 2022 10:44:28 GMT )
Sep 01, 2022 10:44 UTC

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ahul Bayt AS- yaani watu wa nyumba ya Mtume Muhammad SAW, ni ufunguo wa Umoja wa Kiislamu na chimbuko la matumaini katika jamii ya mwanadamu.

Rais Sayyid Ebrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo alipohutubia Kongamano la Saba la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt (as) mjini Tehran.

Rais wa Iran amebaini kuwa leo mwanadamu amepoteza uadilifu na kuongeza kuwa, Ahul Bayt (as) ni siri ya kupigania uadilifu  duniani. Ameendelea kusema kuwa: "Uadilifu ni kitu kilichojikita katika nafsi na asili ya wanadamu wote."

Raisi amesema: "Ulimwengu unazingatia kwa njia maalumu fikra za Ahul Bayt kwani fikra hii ni ya haki na uadilifu, ubinaddamu na mantiki kamili."

Rais wa Iran amesema vijana hasa katika nchi za Magharibi wanaelekea kwa wingi katika dini na umaanawi na kadhia hii inamaanisha kuwa wanaozuoni waliokusanyika katika kongamano hilo wana jukumu kubwa.

Rais Sayyid Ebrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akihutubu katika Kongamano la Saba la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS

Aidha rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ahul Bayt AS ndio ufungua wa wema na ni nembo ya mema mbali na kuwa dhihirisho la ubora wa dunia sambamba na kuwa ufunguo wa sayansi, elimu, maadili, haki na umaanawi wa wanadamu.

Kwingineko katika hotuba yake, Raisi amesema uhusiano wa kielimu, kiutamaduni na kijami baina ya wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt (as) unaweza kuibua mustakabali mwema na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuratibu uhusiano huo.

Kongamano la Saba la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS litajadili masauala ya vyombo vya habari, intaneti, familia, wanawake na uchumi. 

Tags