Jun 11, 2016 15:30 UTC
  • Vikao 400 vya  Qur'ani Tukufu kufanyika kote nchini Iran

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandaa vikao 400 maalumu vya usomaji Qur'ani kote nchini katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamedokezwa na Sayyid Mustafa Husseini, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Awqaf ambaye ameongeza kuwa, vikao hivyo vitahudhuriwa na maqarii sita wa kimataifa kutoka Misri pamoja na maqarii mashuhuri wa kimataifa Wairani.

Sayyid Mustafa Husseini ameongeza kuwa, taasisi za kielimu, kiutamaduni na kisayansi zinahusika katika mahafali na jalsa za kuimarisha ukuruba na mapenzi na Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa ratiba, mwaka huu sawa na miaka iliyopita, kutakuwa pia na vikao vya qasida katika mahafali hizo za usomaji Qur'ani Tukufu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipatia umuhimu mkubwa suala la kuimarisha utamaduni wa Qur'ani kupitia kuandaa programu mbali mbali kama vile maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka mjini Tehran katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa Rajab. Aidha kitaifa hufanyika harakati mbali mbali zinazohusiana na Qur'ani Tukufu.

 

Tags