Jun 12, 2016 03:57 UTC
  • Vikao 400 vya  Qur'ani Tukufu kote Iran

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandaa vikao 400 maalumu vya usomaji Qur'ani kote Iran katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamedokezwa na Sayyid Mustafa Husseini Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu ambaye ameongeza kuwa, vikao hivyo vitahudhuriwa na maqarii sita wa kimataifa kutoka Misri pamoja na maqarii mashuhuri wa kimataifa Wairani.

Sayyid Mustafa Husseini ameongeza kuwa, taasisi za kielimu, kiutamaduni na kisayansi zinahusika katika mahfali na jalsa za kuimarisha ukuruba na kufarijika na Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mipangilio iliyopo, mwaka huu sawa na miaka iliyopita, katika mahafali hizo za kusoma Qur'ani Tukufu pia kutakuwa na vikao vya qasida.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipatia umuhimu mkubwa suala la kuimarisha utamaduni wa Qur'ani kupitia kuandaa programu mbali mbali kama vile maonyesho ya kimatiafa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka mjini Tehran katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa Rajab. Aidha kitaifa hufanyika harakati mbali mbali zinazohusiana na Qur'ani Tukufu.

Tags