Biashara baina ya Iran na Afrika yaongezeka kwa asilimia karibu 40
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91518-biashara_baina_ya_iran_na_afrika_yaongezeka_kwa_asilimia_karibu_40
Naibu afisa wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Iran-Afrika amesema kuwa biashara kati ya Iran na Afrika imestawi kwa asilimia 40.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 10, 2022 04:42 UTC
  • Biashara baina ya Iran na Afrika yaongezeka kwa asilimia karibu 40

Naibu afisa wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Iran-Afrika amesema kuwa biashara kati ya Iran na Afrika imestawi kwa asilimia 40.

Sayyid Ruhullah Latifi, Naibu Mwenyekiti wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Iran na Afrika ametangaza kuwa biashara (jumla ya kuagiza na kuuza nje) bidhaa baina ya Iran na Afrika ilikuwa dola bilioni moja na milioni 56 katika miezi minane ya mwaka huu wa Hijria Shamsia, na kwamba imestawi na kuongezeka kwa asilimia 39 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. 

Hii ni kutokana na sera za Serikali ya 13 ya Jamhuri ya Kislamu za kutoa kipaumbele kwa suala la kupanua zaidi uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za Kiafrika.

Latifi amesema, Afrika Kusini, Msumbiji na Sudan ndizo sehemu tatu zilizoongoza kwa mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika katika kipindi hicho.

Naibu afisa wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Iran-Afrika amesema kuhusu uagizaji bidhaa kutoka Afrika kwamba, tani elfu 69 na 31 za bidhaa zenye thamani ya dola milioni 66 ziliingizwa nchini Iran kutoka nchi 21 za Afrika katika miezi minane ya kwanza ya mwaka, na kwamba kiwango hicho kimeongozeka kwa asilimia 77 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Katika kipindi hicho, Tanzania, Kenya na Afrika Kusini kwa utaratibu zilikuwa nchi tatu zilizoongoza za Kiafrika kuuza bidhaa nyingi zaidi kwa Iran.