Kuwasili nchini Iran ujumbe wa kiuchumi wa Senegal
(last modified Thu, 23 Feb 2023 07:37:46 GMT )
Feb 23, 2023 07:37 UTC
  • Kuwasili nchini Iran ujumbe wa kiuchumi wa Senegal

Ujumbe wa ngazi ya juu wa kiuchumi wa Senegal ukiongozwa na mshauri mkuu wa rais na mkuu wa chama cha wafanyakazi cha nchi hiyo umeasili mjini Tehran.

Biashara kati ya Iran na Senegal mwaka uliopita ilifikia thamani ya dola milioni 2 na laki nne, ambapo asilimia 50 ni sehemu ya mauzo ya vipuri vya magari na pikipiki na asilimia 17 ya hiyo ni sehemu ya mauzo ya bidhaa za chakula nje ya nchi. Vilevile kiasi cha uagizaji bidhaa kutoka Senegal kuja Iran katika muda huo kilikuwa cha karibu dola laki 3.7.

Kuhusiana na hilo, Seyed Ruhollah Latifi, makamu mwenyekiti na msemaji wa jumuiya ya biashara kati ya Iran na Afrika, amesema kuhusu ziara ya ujumbe wa kibiashara wa Senegal nchini Iran kwamba ujumbe huo utakutana kwa muda wa siku 10 na mashirika ya kibiashara na uzalishaji ya Iran, wasimamizi wa vitengo vya uzalishaji na maafisa wanaohusika na biashara ya eneo la Afrika Magharibi ili kuongeza mabadilishano ya biashara chini ya uenyekiti wa "Sheikh Sisse", mshauri mkuu wa masuala ya uchumi wa rais wa Senegal na mkuu wa chama cha wafanyakazi cha nchi hiyo.

Senegal ni nchi yenye wakazi milioni 17 inayopatikana Afrika Magharibi, ambapo asilimia 90 ya raia wake ni Waislamu. Nchi hiyo yenye ukubwa wa kilomita mraba 200,000 inapakana na Mauritania, Mali, Guinea, Guinea-Bissau na Bahari ya Atlantiki, na ni lango la kuingiza bidhaa katika nchi 15 za Afrika ambazo hutoza ushuru mdogo sana wa kuagiza bidhaa. Nchi hiyo inachukuliwa kuwa fursa nzuri kwa ajili ya wafanyabiashara kuingiza bidhaa zao katika nchi za Afrika. Mapato ya nchi hiyo yanatokana na kilimo, viwanda na huduma na njugu karanga, mtama na mahindi ni miongoni mwa mazao ya kilimo ya nchi hiyo.