Russia yarekebisha msimamo wake kuhusu visiwa vitatu vya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i99924-russia_yarekebisha_msimamo_wake_kuhusu_visiwa_vitatu_vya_iran
Mwakilishi maalumu wa Rais wa Russia katika masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika amesisitiza misimamo thabiti ya nchi yake kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba ni nchi rafiki na kwamba Moscow inaheshimu mamlaka na umoja wa ardhi yote ya Iran.
(last modified 2025-11-03T16:45:17+00:00 )
Jul 15, 2023 03:26 UTC
  • Russia yarekebisha msimamo wake kuhusu visiwa vitatu vya Iran

Mwakilishi maalumu wa Rais wa Russia katika masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika amesisitiza misimamo thabiti ya nchi yake kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba ni nchi rafiki na kwamba Moscow inaheshimu mamlaka na umoja wa ardhi yote ya Iran.

Kwa mujibu wa shirikia la habari la IRNA, Mikhail Bogdanov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na mwakilishi Maalumu wa Rais wa Russia katika Masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika, amekutana na Balozi wa Iran mjini Moscow Kazem Jalali jana Ijumaa kujibu habari zilizotangazwa kuhusiana na mkutano wa pamoja wa hivi karibuni wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na Russia, na kusisitiza juu ya misimamo thabiti ya nchi yake kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni nchi rafiki na kwamba Moscow inaheshimu mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi yote ya Iran.

Visiwa vitatu vya Iran vilivyoko katika Ghuba ya Uajemi

Katika taarifa ya hivi karibuni ya kikao cha pamoja cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi GCC na Russia kilichofanyika mjini Moscow, washiriki waliunga mkono juhudi za Muungano wa Falme za Kiarabu, UAE za kutafuta suluhisho la amani la kutatua suala la visiwa vitatu vya Tunb Kubwa, Tunb Ndogo na BoMousa kwa mazungumzo baina ya nchi mbili au kupitia jumuiya za kimataifa.

Suala hilo limekabiliwa na malalamiko rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Russia; na mbali na msimamo uliotangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje na baadhi ya maafisa wa Iran, balozi wa Russia mjini Tehran aliitwa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na kukabidhiwa taarifa ya malalamiko ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na yaliyomo kwenye taarifa ya pamoja ya Moscow na GCC.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwakilishi maalumu wa Rais wa Russia katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika na balozi wa Iran mjini Moscow wamebadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo hali ya sasa ya uhusiano wa pande mbili kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia.../