-
Mohsein Rezaei: Israel inaharakisha anguko lake kwa kuwauwa makamanda wa Muqawama
Nov 24, 2025 11:53Kamanda Mkuu wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kuwa mauaji yanayofanywa na utawala wa Israel dhidi ya makamanda wa Muqawama yanaharakisha kuangamia utawala huo.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wafanya mazungumzo mjini Muscat
Nov 24, 2025 03:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi amekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Oman Badr Al-Busaidi mjini Muscat Jumapili jioni na kujadili masuala mbalimbai yakiwemo ya uhusiano wa pande mbili na matukio muhimu ya kikanda.
-
Danny Citrinowicz: Ushawishi wa vyombo vya habari vya Iran barani Afrika umeongezeka
Nov 24, 2025 03:44Mtafiti mkuu wa Mpango wa Iran katika Taasisi ya Utafiti wa Usalama wa Taifa ya Israel (INSS) ameeleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa ushawishi wa vyombo vya habari vya Iran barani Afrika na matokeo yake ya muda mrefu dhidi ya maslahi ya utawala wa Kizayuni barani humo.
-
Tehran: Azimio la IAEA dhidi ya Iran ni 'doa la fedheha' kwa watayarishaji wake
Nov 23, 2025 23:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani azimio lililopitishwa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kuhusu mpango wa amani wa nyuklia wa Tehran na kulitaja kuwa "doa la fedheha" kwa wafadhili wa azimio hilo.
-
Iran yaidhinisha miradi ya uwekezaji wa kigeni ya dola milioni 485
Nov 23, 2025 23:33Bodi ya uwekezaji wa kigeni ya Iran imeidhinisha maombi 67 yenye thamani ya dola milioni 485 wakati wa mkutano wake wa tisa wa mwaka, kuashiria maslahi mapya kutoka kwa wawekezaji wa kimataifa katika sekta nyingi.
-
Iran: Utawala wa kizayuni hauna mpaka katika kutenda jinai
Nov 23, 2025 08:36Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala haramu wa Israel hauna mpaka katika kutenda jinai na wqala hauheshimu ahadi wala sheria yoyote ya kimataifa.
-
Kamanda: Jeshi la Iran liko tayari kukabiliana na tishio lolote
Nov 22, 2025 23:42Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Iran, akizungumza mbele ya makamanda wenzake, amesisitiza kuwa kwa kuzingatia maelekezo ya Kiongozi Muadhamu na kwa kutumia tajiriba ya vita vya zamani, hususan vita vya kulazimishwa vya siku 12 vya mwezi Juni, jeshi limeweka mkakati wa kuzingatia nguzo tano: utii wa uongozi, uadilifu, ufanisi, teknolojia na uboreshaji wa ujuzi.
-
Madini ya risasi na zinki yaimarisha hadhi ya Iran kama ngome ya madini Asia Magharibi
Nov 22, 2025 23:37Tarehe 22 Novemba, huadhimishwa kitaifa nchini Iran kama Siku ya Madini ya Risasi na Zinki ikiwa ni kuashiria nafasi kuu ya sekta hii na uhusiano wake wa karibu na malengo ya kiuchumi ya taifa.
-
Marekani na nchi tatu za Ulaya zimeuaje Mkataba wa Cairo?
Nov 22, 2025 23:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika kwenye akaunti yake ya X kwamba: ""Mkataba wa Cairo" umeangamizwa na Marekani na nchi tatu za Ulaya."
-
Harakati ya pamoja ya kupinga hatua ya Magharibi dhidi ya Iran katika Bodi ya Magavana ya IAEA
Nov 22, 2025 06:50Hivi sasa kumejitokeza harakati ya pamoja ya kupinga hatua ya Troika ya Ulaya na Marekani dhidi ya Iran katika Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).