-
Abu Hatab wa Ghaza asimulia alivyoshiriki kuzika Wapalestina 18,000 waliouliwa kinyama na Israel
Dec 23, 2025 08:32Mzikamaiti Yousef Abu Hatab mkazi wa Ukanda wa Ghaza na mmoja wa mashuhuda wa moja ya majanga makubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Palestina, amesema ameshiriki kuzika karibu miili 18,000 ya Wapalestina waliouliwa shahidi wakati wa vita vya kinyama na vya mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel katika eneo hilo la Palestina.
-
Vence adai Ulaya itakuwa hatari kwa Marekani, kwa kuwa eti itatawaliwa na Waislamu
Dec 23, 2025 08:26Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance amedai kuwa, Ulaya Magharibi yenye silaha za nyuklia inaweza kuwa hatari kubwa ya kiusalama kwa Marekani ikiwa utambulisho wa kitaifa wa nchi zake utaendelea kubadilika kutokana na uhamiaji mkubwa unaofanyika katika nchi hizo.
-
Kuzidi kuwa tata vita vya Sudan; indhari ya Umoja wa Mataifa kuhusu kupanuka wigo wake
Dec 23, 2025 08:24Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa sanjari na kusisitiza umuhimu wa kusitisha vita nchini Sudan, ameonya kuhusu utambulisho wake tata na athari zake zinazopanuka kwa nchi jirani na eneo kwa ujumla.
-
Pakistan kumuuzia silaha Haftar wa Libya za dola bilioni 4 zikiwemo ndege za kivita za China
Dec 23, 2025 08:09Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa, Pakistan imesaini makubaliano yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 4 ya kuuza zana za kijeshi, ikiwa ni pamoja na ndege za kivita zilizoundwa na nchi hiyo kwa kushirikiana na China, kwa kundi liitwalo Jeshi la Taifa la Libya (LNA)LNA linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar, mmoja wa wababe wakuu wa kivita nchini humo.
-
Sambamba na kuanza tena chokochoko za Trump, EU yasema iko pamoja na Denmark, Greenland
Dec 23, 2025 07:48Umoja wa Ulaya umeonyesha mshikamano na Denmark na eneo la Greenland kufuatia tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuteua mjumbe wake maalumu katika eneo hilo.
-
Sudan yapendekeza usitishaji mapigano kamili chini ya usimamizi wa kikanda na kimataifa
Dec 23, 2025 04:39Waziri Mkuu wa Sudan, Kamil Idris jana Jumatatu, alihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuwasilisha mpango ambao unajumuisha usitishaji mapigano kamili chini ya usimamizi wa kikanda na kimataifa, akisisitiza kwamba Sudan imelipa gharama kubwa kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo.
-
Makundi ya kiraia A/Kusini yataka kupewa dhamana wanaharakati wa Palestina waliogoma kula katika jela za UK
Dec 23, 2025 04:38Makundi kadhaa ya kiraia nchini Afrika Kusini yametoa wito yakitaka kupewa dhamana haraka iwezekanavyo wanaharakati wawili watetezi wa Palestina waliogoma kula katika jela za Uingereza yakisema kuwa kuendelea kufungwa raia hao kunahatarisha maisha yao.
-
Venezuela yataka kuhitimishwa uwepo kijeshi wa Marekani katika eneo la Caribbean
Dec 23, 2025 04:33Venezuela imetoa wito wa "kusitishwa mara moja" utumaji wa wanajeshi wa Marekani katika eneo la Caribbean.
-
Wademocrat wataka kushinikizwa Israel kwa kukiuka usitishaji vita Gaza
Dec 23, 2025 04:30Makumi ya Wademokrat katika Bunge la Marekani wameitaka Ikulu ya Rais wa nchi hiyo (White House) kuushinikiza kidiplomasia utawala wa Israel ili usitishe ukiukaji wa mapatano ya kutisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
-
Ndege za kijasusi za Marekani zaruka katika maeneo mbalimbali ya Nigeria
Dec 23, 2025 04:23Ndege za Marekani zimekuwa zikipataa katika maeneo mengi ya Nigeria kwa lengo la kukusanya taarifa za kijasusi tangu mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.