-
Araghchi na Guterres wajadili migogoro ya Gaza, Yemen
Oct 21, 2025 08:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres wamefanya mazungumzo ya simu na kuzungumzia matukio ya kikanda ikiwemo hali ya Gaza na Yemen.
-
Hamas: Israel lazima igharamie ujenzi mpya wa Gaza
Oct 21, 2025 08:01Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, Mousa Abu Marzouk ametoa wito kwa Israel kufadhili kikamilifu ukarabati na ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza, akitaja uharibifu mkubwa na haki za Wapalestina zaidi ya milioni mbili ambao wamepoteza makazi yao, makazi na riziki.
-
Trump: Ukraine haiwezi kushinda vita dhidi ya Russia
Oct 21, 2025 07:56Rais wa Marekani, Donald Trump amesema haitakidi kwamba Ukraine inaweza kuibuka mshinda katika vita vyake na Russia.
-
Uwanja wa Ndege Khartoum washambuliwa na RSF kabla ya kufunguliwa
Oct 21, 2025 07:29Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vimeripotiwa kushambulia maeneo muhimu katika mji mkuu wa Sudan, ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo.
-
Qur'ani inasema nini kuhusu watu wenye kiburi kama Donald Trump
Oct 21, 2025 06:51Uchambuzi wa Qur'ani kuhusu tabia ya Donald Trump, rais mtata wa Marekani, unamuonyesha kuwa ni mfano wa wazi wa mtu muovu na mwenye kutakabari.
-
Hizbullah: Trump anajiona mtu wa amani ilhali ni gaidi namba moja duniani
Oct 21, 2025 03:32Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Siasa la Hizbullah amesisitiza kuwa, Rais wa Marekani anajiona ni “mtu wa amani” duniani ilhali kiuhalisia yeye ni “mchekeshaji, muigizaji, mdanganyifu na mzandiki, na ndiye gaidi namba moja duniani” aliyemuua shahidi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyed Hassan Nasrullah (Radhi za Allah ziwe juu yake), kwa mabomu ya Marekani.
-
Iraq: Hatutaruhusu ardhi na anga yetu zitumike kutishia usalama wa Iran, majirani wengine
Oct 21, 2025 03:31Iraq iimesisitiza kuwa haitaruhusu ardhi na anga yake zitumike kutishia usalama wa Iran au wa nchi nyingine yoyote jirani.
-
Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Madagascar amteua mfanyabiashara kuwa waziri mkuu mpya
Oct 21, 2025 03:31Rais wa mpito wa Madagascar Kanali Michael Randrianirina amemteua mfanyabiashara Herintsalama Rajaonarivelo kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo na kumuapisha katika hafla rasmi iliyofanyika kwenye Ikulu ya Jimbo la Iavoloha.
-
Amir wa Qatar: Vita vya Israel dhidi ya Ghaza si kingine chochote ila ni mauaji ya kimbari
Oct 21, 2025 03:30Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amesema, vita vya utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza si kitu kingine ila ni mauaji ya kimbari sambamba na kuulaani utawala huo ghasibu kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Netanyahu ajigamba kuwa siku ya Jumapili Israel iliidondoshea Ghaza tani 153 za mabomu
Oct 21, 2025 03:30Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amejigamba kuwa jeshi lake lilishambulia Ukanda wa Ghaza siku ya Jumapili kwa tani 153 za mabomu, ambayo ni sawa na kukiri kwamba utawala huo ghasibu umekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano uliyofikia na harakati ya Hamas kupitia mpango uliopendekezwa na Rais wa Marekani.