-
Bunge la Uhispania laidhinisha marufuku ya kuuuzia silaha utawala wa kizayuni wa Israel
Oct 09, 2025 07:08Bunge la Uhispania limeidhinisha vikwazo vya silaha vilivyopendekezwa na Waziri Mkuu Pedro Sanchez dhidi ya utawala wa kizayunii wa Israel.
-
Upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati: Hatutashiriki uchaguzi mkuu wa Desemba 28
Oct 09, 2025 07:07Upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umetangaza kuwa utasusia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Disemba ambapo Rais Faustin-Archange Touadera atawania tena urais kwa muhula wa tatu.
-
Chama tawala Italia kuwasilisha muswada wa kupiga marufuku uvaaji burqa na niqabu maeneo ya umma
Oct 09, 2025 07:03Gazeti la Politico la nchini Italia limeripoti kuwa chama tawala nchini humo cha Brothers of Italy kimesema, kinapanga kuwasilisha mswada bungeni wa kupiga marufuku wanawake wa Kiislamu kuvaa vazi la burqa na niqabu katika maeneo ya umma, kikitaja sababu ya kufanya hivyo kuwa ni kupinga ilichokiita "utengano wa Kiislamu".
-
Iran, Russia zajadili kuendeleza ushirikiano wa nyuklia
Oct 09, 2025 03:45Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amekutana na kuzungumza mjini Tehran na afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Taifa la Nishati ya Atomiki la Russia( Russia Rosatom) na kujadili kustawisha ushirikiano katika uga wa nishati ya nyuklia yenye malengo ya amani kati ya nchi mbili hizo waitifaki.
-
Wanaharakati wa Afrika Kusini katika msafara wa Sumud; Tulimkaripia Waziri wa Israel tukiwa kizuizini
Oct 09, 2025 03:44Wanaharakati sita wa Afrika Kusini ambao waliwekwa kizuizini huko Israel baada ya kutekwa nyara kutoka katika msafara wa kimataifa wa meli kwa jina la Global Sumud Flotilla kuelekea Gaza wamesimulia hadithi za kusikitisha kuhusu walichopitia wakiwa mikononi mwa wanajeshi wa Israel.
-
Wanamgambo wa RSF washambulia hospitali jimboni Darfur; watu 12 wameuawa, 17 kujeruhiwa
Oct 09, 2025 03:44Raia wasiopungua 12 wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika jimbo la Darfur Kaskazini.
-
Rais wa Madagascar afanya mazungumzo licha ya waandamanaji kususia
Oct 09, 2025 03:43Rais Andry Rajoelina wa Madagascar jana aliyaalika makundi na asasi kadhaa za kiraia kwa ajili ya mazungumzo katika ikuu ya Rais.
-
Ethiopia yaituhumu Eritrea kuwa inajiandaa kuanzisha vita dhidi yake
Oct 09, 2025 03:43Ethiopia imeituhumu Eritrea kuwa inajiandaa kuanzisha vita dhidi yake. Ethiopia imetoa tuhuma hizi dhidi ya Eritrea ikiwa ni ishara ya karibuni ya kushtadi mvutano katika nchi mbili hizo jirani kuhusu udhibiti wa Bahari Nyekundu.
-
Israel yaendelea kufanya jinai Ghaza licha ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita
Oct 08, 2025 23:44Duru mbalimbali za kieneo zimeripoti mepema leo Alkhamisi kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kufanya mashambulizi makali katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Ghaza licha ya kufikiwa makubaliano ya kusimamisha vita.
-
IRGC yaonya; Jibu kali litawakabili maadui 'wakikosea' katika Ghuba ya Uajemi, Hormuz
Oct 08, 2025 23:44Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kuwa, hatua zozote za makosa zitakazofanywa na maadui katika Ghuba ya Uajemi, Lango Bahari la Hormuz au katika visiwa vya Iran, zitakabiliwa na jibu kali na la kujutisha.