-
IRGC yaonya; Jibu kali litawakabili maadui 'wakikosea' katika Ghuba ya Uajemi, Hormuz
Oct 08, 2025 23:44Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kuwa, hatua zozote za makosa zitakazofanywa na maadui katika Ghuba ya Uajemi, Lango Bahari la Hormuz au katika visiwa vya Iran, zitakabiliwa na jibu kali na la kujutisha.
-
ICC yazitaka nchi wanachama kutekeleza hati za kukamatwa Netanyahu, Gallant
Oct 08, 2025 23:43Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Fadi El Abdallah ameiambia kanali ya Al-Jazeera kwamba, nchi wanachama wa Mkataba wa Roma zina wajibu wa kisheria kushirikiana na mahakama hiyo katika kutekeleza waranti wa kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na aliyekuwa Waziri wa Vita wa utawala huo pandikizi, Yoav Gallant.
-
Jihadul Islami: Mpango wa Trump kwa Gaza unalenga kuwapigisha magoti Wapalestina
Oct 08, 2025 23:42Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina ya Jihadul Islami amesema kuwa, mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani wa eti kusimamisha vita Gaza unaupendelea tu utawala wa Kizayuni, na unalenga kuwafanya Wapalestina wasalimu amri.
-
Jeshi la Pakistan launga mkono bila ya masharti kuasisiwa nchi huru ya Palestina
Oct 08, 2025 23:42Makamanda wa jeshi la Pakistan wamebainisha matarajio yao kuhusu kusitishwa vita haraka iwezekanavyo huko Gaza na kutumwa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo na kusisisitiza kuwaa Pakistan inaendelea kuunga mkono bila masharti suala la kuasisiwa nchi huru ya Palestina.
-
ICRC: Mgogoro wa afya Kongo DR unazidi kuwa mbaya
Oct 08, 2025 23:41Mfumo wa huduma za afya katika eneo linalokumbwa na migogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umezorota kwa kiasi kikubwa, huku vituo vingi vya matibabu vikiwa na uhaba mkubwa wa dawa na wafanyakazi, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imeonya katika taarifa yake ya jana Jumatano.
-
Misri na vita vya Gaza; Kujaribu kufuata mkakati wa uwastani
Oct 08, 2025 23:40Kuanza vita vya Gaza baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo Oktoba 7, 2023 ulikuwa mwanzo wa mabadiliko katika sera za ndani na za kigeni za Misri.
-
Pezeshkian: Iran ipo tayari kuimarisha uhusiano na Ivory Coast
Oct 08, 2025 09:15Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imejiandaa kikamilifu kupanua ushirikiano wa pande mbili na Ivory Coast ili kufikia malengo ya pamoja.
-
Jeshi la majini la Iran lasaini hati ya ushirikiano wa kimkakati na nchi za eneo la Kaspi zenye ukanda wa pwani
Oct 08, 2025 08:59Makamanda wa majeshi ya majini ya Iran, Russia, Kazakhstan na Azerbaijan wametia saini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati unaolenga kuimarisha usalama katika maji ya pamoja.
-
Somalia yakanusha vikali kufikia makubaliano ya siri na Sweden kuhusu kuwarejesha nchini raia wake
Oct 08, 2025 08:58Ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia leo imetoa taarifa na kukadhibisha vikali Somalia kwamba imefikia makubaliano ya siri na Sweden kuhusu kuwarejesha nyumbani raia wa Somalia kutoka Sweden ukiwemo pia mpango wa msaada wenye masharti kwa Somalia.
-
Kushiriki makundi ya Palestina katika mazungumzo ya Sharm el-Sheikh
Oct 08, 2025 08:58Televisheni ya al Jazeera yenye makao yake mjini Doha Qatar imemnukuu afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina na kuripoti kuwa wawakilishi wa makundi kadhaa ya Wapalestina wamejiunga na timu za mazungumzo huko Sharm el-Sheikh Misri hatua waliyoitaja kuwa yenye lengo la kufanikisha matakwa ya wananchi wa Palestina.