Kushiriki makundi ya Palestina katika mazungumzo ya Sharm el-Sheikh
Televisheni ya al Jazeera yenye makao yake mjini Doha Qatar imemnukuu afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina na kuripoti kuwa wawakilishi wa makundi kadhaa ya Wapalestina wamejiunga na timu za mazungumzo huko Sharm el-Sheikh Misri hatua waliyoitaja kuwa yenye lengo la kufanikisha matakwa ya wananchi wa Palestina.
Chanzo cha habari katika safu ya uongozi ya Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina kimeiambia televisheni ya al Jazeera kwamba jumbe za mazungumzo wakiwemo wawakilishi wa Jihadul Islami na Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina wamejiunga na timu za mazungumzo huko Sharm el Sheikh.
Chanzo hicho cha habari kimeeleza kuwa jumbe za makundi ya zina jukumu la kuhakikisha kuwa makubaliano yanafikiwa ili kuhitimisha masaibu na mateso ya wananchi wa Palestina na kukomesha mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina.
Chanzo hicho cha habari aidha kimesisitiza kuwa makundi ya Palestina yanataka kuhitimishwa vita kuondoka kikamilifu wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel huko kama kama vipaumbele vya wananchi wa Palestina.
Imeongeza kuwa, kushiriki katika mazungumzo ya Sharm el Sheikh Misri makundi mengine ya Palestina pamoja na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ni takwa la kitaifa la Palestina; hatua abayo hatua ambayo imekaribishwa na kuungwa mkono pia na wapatanishi.