-
Marekani ilishindwa vipi katika vita dhidi ya Iran?
Jun 16, 2026 06:29Siku mia moja na sita baada ya kuanza hujuma za kijeshi za Marekani na Wazayuni dhidi ya Iran, hatimaye Tehran na Washington zimefikia muafaka katika mfumo wa makubaliano ya kuhitimisha rasmi vita hivyo.
-
Iran yatoka sare ya mabao 2 kwa 2 na New Zealand, Misri yagawana pointi na Ubelgiji Kundi G
Jun 16, 2026 05:53Timu ya Taifa ya Iran, Team Melli, imetoka sare ya mabao mawili kwa mawili na timu ya taifa ya New Zealand katika mechi ya kundi G iliyopigwa uwanja wa SoFi Stadium huko California.
-
Pezeshkian: Hasira ya Israel dhidi ya MoU na Marekani ni 'ishara dhahiri' ya ushindi wa Iran
Jun 16, 2026 03:23Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema hasira ya Israel kuhusu hati ya maelewano (MoU) ya makubaliano kati ya Iran na Marekani inaashiria wazi mafanikio na ushindi wa taifa la Iran.
-
Ayatullah Amoli Larijani: Istiqama ya taifa imeshinda 'kiburi kibaya cha US-Israel
Jun 16, 2026 02:59Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu istiqama na ushujaa wa taifa kubwa la Iran mbele ya "kiburi kibaya" cha Marekani na utawala wa Israel.
-
Waziri Mkuu: Pakistani itakuwa mwenyeji wa hafla ya "kihistoria" ya kusaini makubaliano ya Iran na Marekani mjini Geneva, Juni 19
Jun 16, 2026 02:57Waziri Mkuu wa Pakistani, Shehbaz Sharif amesema kuwa hafla ya kutia saini Mkataba wa Maelewano kati ya Iran na Marekani (MOU) itaandaliwa na nchi yake mjini Geneva, Juni 19 mwaka huu.
-
Baada ya Trump kusherekea bethidei yake ya 80, sasa umri na afya ndio kiini cha mjadala wa kisiasa wa Marekani
Jun 16, 2026 02:53Ripoti ya Newsweek inaonyesha kwamba kutimiza umri wa miaka 80 Rais wa Marekani Donald Trump kumerejesha mjadala wa umri na afya ya rais katika mstari wa mbele wa malumbano ya kisiasa nchini Marekani, baada ya yeye mwenyewe kufanya umri na utimamu wa akili wa mtangulizi wake, Joe Biden kuwa moja ya mada kuu za kampeni yake ya uchaguzi.
-
Tel Aviv inawakera hata washirika wake, Ufaransa yalituhumu shirika la Israel kuingia mambo ya ndani ya nchi hiyo
Jun 16, 2026 02:52Baada ya takriban mwezi mmoja wa uchunguzi rasmi, Paris imeituhumu kampuni ya Israel kwa kuingilia uchaguzi uliopita nchini Ufaransa, na imetaka maelezo kutoka Tel Aviv kuhusu suala hilo.
-
Uingereza kupiga marufuku watoto wa chini ya miaka 16 kutumia mitandao ya kijamii
Jun 16, 2026 02:47Waziri Mkuu wa Uingereza jana alisema nchi hiyo itapiga marufuku watoto walio na umri wa chini ya miaka 16 kutumia programu mbalimbali za mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Snapchat, TikTok na YouTube ili kuwalinda vijana dhidi ya maudhui hatari na kupoteza muda mwingi katika mitandao ya kijamii.
-
Trump afedheheka kwa kusherehekea kurejea katika hali ya kabla ya vita na Iran
Jun 15, 2026 13:56Wataalamu wengi wa masuala ya siasa wametathmini utangulizi wa mapatano ya kusitisha vita kati ya Marekani na Jamhuri ya Kislamu ya Iran na kuyataja kuwa fedheha kubwa kwa utawala wa Marekani unaoongozwa na Rais Donald Trump.
-
Kamishna wa Haki za Binadamu UN: Mapigano yasitishwe Gaza na Lebanon, aonya kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan
Jun 15, 2026 12:26Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza haja ya kuimarishwa usitishaji mapigano huko Gaza na kufikiwa makubaliano endelevu ya kusitisha mapigano, akibainisha kuwa vikosi vya jeshi la Israel vimewaua Wapalestina wapatao 1,000 tangu usitishaji mapigano Oktoba mwaka jana, pamoja na kuimarisha vizingiti vya kuzuia misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza, jambo ambalo amesema limezidisha mgogoro wa binadamu katika sekta hiyo.