Israel na Somaliland: Njama ya kudhibiti Bab al Mandeb
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137906-israel_na_somaliland_njama_ya_kudhibiti_bab_al_mandeb
Tarehe 26 Desemba, 2025, Israel ililitambua eneo lililotangaza kujitenga na Somalia la Somaliland kama taifa huru; licha ya kwamba, katika upeo wa kimataifa, eneo hilo inaendelea kutambuliwa kuwa sehemu ya Somalia.
(last modified 2026-04-23T10:06:54+00:00 )
Apr 23, 2026 09:59 UTC
  • Bab al Mandab
    Bab al Mandab

Tarehe 26 Desemba, 2025, Israel ililitambua eneo lililotangaza kujitenga na Somalia la Somaliland kama taifa huru; licha ya kwamba, katika upeo wa kimataifa, eneo hilo inaendelea kutambuliwa kuwa sehemu ya Somalia.

Umuhimu wa hatua hii unapaswa kuonekana katika nafasi ya kijiopolitiki ya Somaliland; ukanda nyeti unaounganisha Mediterania, Mashariki ya Kati, na Bahari ya Hindi.

Katika anga ya baada ya Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa, uamuzi huu unaonekana zaidi kuwa ni ishara ya jitihada za Israel za kutumia ombwe la kijiopolitiki na kupanua ushawishi wake katika Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu, kuliko hatua ya kawaida ya kidiplomasia.

Wasiwasi kuhusu washirika wa Iran, haswa harakati ya Ansarullah ya Yemen, umetumika kama kisingizio cha kuendelezwa sera hiyo ya Israel. Kuwa na uhusiano na Somaliland yumkini kukaiwezesha Israel kuanzisha miundombinu ya ujasusi na usalama karibu na Yemen, ambapo mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za wapiganaji wa al Houthi hupita.

Kwa mtazamo wa kimkakati, Somaliland iko katika nafasi nzuri ya kudhibiti na kufuatilia safari za baharini na mawasiliano ya kupitia chini ya maji kutokana na kuwa kwenye mojawapo ya njia muhimu zaidi za baharini duniani. Katika muktadha huu, kutambua rasmi eneo hilo kama nchi inayojitawala huonekana kama jaribio la kupata kituo cha ufuatiliaji katika mojawapo ya maeneo nyeti zaidi duniani; hatua ambayo badala ya kuchangia utulivu wa kikanda, inatumika kuimarisha usalama na harakati za ujasusi za Israel.

Katika kiwango cha uchambuzi, hatua hiyo ya Israel ni kielelezo cha mbinu ya kuingilia kati masuala ya mataifa mengine; zikiwa ni jitihada za kulazimisha ushawishi kwa kuhalalisha jambo linaloibua utata mkubwa na kutumia vibaya migawanyiko ya kiutawala barani Afrika. Sera kama hiyo sio tu kwamba zinadhoofisha kanuni za sheria za kimataifa, lakini pia, zinazidisha ukosefu wa amani na usalama katika maeneo ya Bahari Nyekundu na kuandaa mazingira ya migogoro mikubwa zaidi kwa kugeuza maeneo yenye mivutano kuwa uwanja wa mashindano ya niaba.

Kwa kuhalalisha dola lisilo halali huko Somaliland, Israel inataka kuzidisha uwezo wake wa kufuatilia shughuli za harakati ya Ansarullah na safari za baharini katika lango muhimu la Bab el Mandeb.

Hata hivyo mienendo hii ya utawala wa Kizayuni itakuwa na taathira nyingi mbaya kwa kanda hiyo ya Afrika, ikiwa ni pamoja na:

1. Kuzidisha mapigano na ukosefu wa amani ndani ya Somalia.

2. Kuchochea harakati za kujitenga katika nchi zingine.

3. Kutengeneza vyanzo vipya vya ukosefu wa amani katika eneo hilo.

4. Kuzidisha uingiliaji kati wa kigeni na migogoro ya kidiplomasia. Na

5. Kuibuka migogoro ya binadamu na kuhama watu kwa kulazimishwa.