Dec 08, 2023 13:56 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Vitendo vya Israel huko Gaza ni uhalifu

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya maafa huko Gaza na kusema kuwa, mashambulizi ya kijeshi ya Israel huko Gaza ni jinai na uhalifu.

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya maafa huko Gaza na kusema kuwa, mashambulizi ya kijeshi ya Israel huko Gaza ni jinai na uhalifu.

Kwa mujibu wa televisheni ya France 24, Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, amesema kuwa: "Hivi sasa, hakuna anayeweza kusaidia kuboresha hali ya mambo, kwa sababu hali ya sasa ni janga kubwa." Amesema, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia alituma ujumbe kama huo takriban miezi miwili iliyopita wakati wa mashambulizi ya kikatili ya Israel Ukanda wa Gaza.   

Albanese ameongeza kuwa: Ukanda wa Gaza ulikuwa ukikabiliwa na mgogoro wa kibinadamu hata kabla ya shambulio la Oktoba 7, kwa sababu umekuwa ukizingirwa tangu miaka kumi na sita iliyopita na umepitia vita tano hadi sasa. Amesema: Baada ya miezi miwili ya mashambulizi makali ambayo yameharibu zaidi ya 60% ya miundombinu ya raia wa Gaza, kuuawa watu baina ya elfu 15 na elfu 20 na kujeruhi zaidi ya wengine elfu 40, wakati ambapo hospitali katika ukanda huo haziwezi tena kuendelea kufanya kazi, hali katika Ukanda wa Gaza imekuwa mbaya sana.

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesema kuwa mashambulizi ya Israel huko Gaza ni za jinai na uhalifu na ameitaka jamii ya kimataifa kutekeleza wajibu wake kuhusiana na suala hilo. 

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Gaza, tangu kuanza kwa uvamizi wa utawala wa Kizayuni katika eneo hilo, watu 17,177 wameuawa shahidi na wengine 46,000 wamejeruhiwa.