Jan 22, 2024 07:31 UTC
  • Mufti wa Oman: Kujitahidi kwa Ukombozi wa Al-Aqsa ni wajibu kwa Waislamu wote

Mufti Mkuu wa Oman kwa mara nyingine amesisitiza umuhimu wa Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel na akasema kuukomboa ni jukumu la Waislamu wote duniani.

Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili aliyasema hayo katika chapisho lake la hivi karibuni katika mtandao wa X, ambalo zamani ulijulikana kama Twitter.

Alisema kama Kibla cha kwanza katika Uislamu na mahali ambapo Mtukufu Mtume (SAW) alianzia Mi’raj (kupaa mbinguni), Al-Aqsa ina umuhimu na thamani kubwa.

Alisema kila Muislamu lazima achukue hatua kuelekea ukombozi wa Palestina, ambao ni wajibu mtakatifu.

Mwanazuoni huyo amesema kutokana na kukaliwa kwa mabavu mji mtakatifu wa al-Quds kwa miongo kadhaa iliyopita, Waislamu katika maeneo tofauti ya dunia wamenyimwa fursa ya kuzuru msikiti huo na kuswali humo.

Aidha amesema kwa sababu ya hujuma ya kitamaduni na kiitikadi ya Magharibi, baadhi ya Waislamu wanaweza kuwa wamesahau haki yao ya kufika mahali hapa patakatifu.

Masjidul Aqsa

Mufti Al Khalili ameongeza kuwa baadhi ya vyombo ya habvari vimetumiwa (na maadui wa Uislamu) kuwaaminisha Waislamu kwamba Msikiti wa Al-Aqsa ni suala linalohusiana na Wapalestina pekee.

Hata hivyo, alibainisha, Operesheni ya Kimbunga Al-Aqsa iliyoanzishwa na vikosi vya muqawama vya Gaza, iliwakumbusha Waislamu wote wajibu wao.

Mufti wa Oman aliendelea kusem ni wakati sasa kwa Waislamu kuweka kando tofauti zao na kujitahidi kurejesha haki zao kwa kuunga.

 

Tags