Apr 30, 2024 11:11 UTC
  • Vituo vya utafiti vya Ulaya vyaiunga mkono Palestina na kuiwekea vikwazo Israel

Vituo vya utafiti barani Ulaya vimeuwekea vikwazo utawala wa Kizayuni na kuunga mkono malengo ya Palestina. Viituo hivyo vya utafiti vya Ulaya pia vimelaani jinai za utawala huo unaotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza.

Katika ripoti yake, Gazeti la Times la Israel limeinukuu Wizara ya Ubunifu, Sayansi na Teknolojia ya utawala wa Kizayuni na kuashiria  hatua ya vituo vya utafiti vya nchi mbalimbali za Ulaya ikiwa ni pamoja na Italia, Ubelgiji, Norway, Denmark, Finland, Sweden, Iceland na Ireland vya kuuwekea vikwazo vya kisayansi vya utawala huo na kuandika kuwa: Ushirikiano wa kimataifa kati ya vituo hivyo na watafiti wa Israel umepungua pakubwa tangu Oktoba 7 mwaka jana hadi sasa kufuatia mauaji ya kimbari ya utawala huo haramu dhidi ya Gaza.

Israel inatekeleza mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza 

Kwa mujibu wa ripoti hiy, asilimia 37 ya miradi ya utafiti ya utawala wa Kizayuni ilikuwa ikifanyika kwa kushirikiana na wasomi wa Ulaya lakini hivi sasa ni vigumu Wazayuni kuzifikia maabara na miundombinu ya utafiti barani Ulaya  huku Wazayuni wakipigwa marufuku kushiriki katika mikutano mingi ya kisayansi ya Ulaya. 

Gazeti la Times la Israel pia limeandika: Miradi ya kiutafiti ya utawala wa Kizayuni katika nyanja za tiba, biolojia, fizikia, anga na sayansi ya kompyuta imeathiriwa na vikwazo hivyo. 

Utawala wa Israel unatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kwa kuunga mkono kwa hali na mali na Marekani mbele ya kimya cha taasisi za kimataifa za kutetea haki za binadamu kwa zaidi ya miezi sita sasa baada ya kuanzisha vita na mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa ukanda huo wasio na hatia. 

 

Tags