May 20, 2021 11:46 UTC
  • Wakuu wengine wawili wa magenge ya kigaidi waangamizwa nchini Yemen

Duru moja ya usalama ya Yemen imetangaza habari ya kuangamizwa wakuu wengine wawili wa magenge ya kigaidi nchini humo.

Televisheni ya Rusia al Yaum imenukuu duru moja ya usalama wa Yemen ikithibitisha habari hiyo na kusema kuwa, viongozi mbalimbali wa makundi ya kigaidi ya Daesh (ISIS) na al Qaida wameshaangamizwa hadi hivi sasa nchini Yemen. Katika matukio ya karibuni zaidi, kiongozi mmoja muhimu wa al Qaida na kamanda mmoja mkubwa wa genge hilo waliangamizwa jana Jumatano nchini humo.

Duru hiyo imemtaja mmoja wa viongozi hao wa magaidi al Qaida kwa jina la Nasir Said al Karami ambaye alikuwa kiongozi wa masuala ya kijasusi na kiusalama wa genge hilo. Magaidi hao wawili wakubwa wameuawa katika mikoa ya Abyan na Shubwah. 

Mpiganaji wa Ansarullah katika medani ya mapambano ya ukombozi wa Yemen

 

Gaidi mwingine amemtaja kwa jina la Saleh Ahmad al Karami ambaye alikuwa kamanda wa kijeshi wa genge la al Qaida nchini Saudi Arabia.

Taasisi ya Usalama na Ujasusi ya  Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen kwa upande wake imeripoti kuwa, nyumba na mashamba yanayotumiwa na magaidi wa al Qaida katika mkoa wa Ma'rib, hoteli na sehemu za kuishi, maghala ya silaha na vifaa vya kijeshi, kambi za mafunzo na njia wanazotumiwa magaidi kwenda na kurudi huko Ma'rib pamoja na wanaofanya uratibu baina yao na muungano vamizi wa Saudia, vyote hivyo vimeshagunduliwa.

Kama tulivyoashiria hivi punde, hadi hivi sasa viongozi wa ngazi za juu wa magenge ya kigaidi ya Daesh na al Qaids wameshaangamizwa au kutiwa mbaroni katika maeneo ya kusini mwa Yemen.

Tags