Jul 21, 2021 07:53 UTC
  • A'saaib Ahlil-Haq: Utawala wa Kizayuni na Marekani ndio waliohusika na mripuko wa Baghdad

Katibu Mkuu wa harakati ya A'saaib Ahlil-Haq ameashiria njama za Marekani za kutaka kuliimarisha genge la DAESH(ISIS) nchini Iraq na akasema: katika kufanikisha jambo hilo, Washington inasaidiwa na mashirika ya intelijensia ya Israel na nchi za Kiarabu.

Qais Khazali amelaani mripuko wa bomu uliotokea kwenye kitongoji cha Sadr mjini Baghdad na kueleza kwamba, Marekani inafanya juu chini ili iendelee kuwepo nchini Iraq kwa njia ya kuliimarisha genge la kigaidi la Daesh.

Khazali amesema, Daesh limeundwa na kutumiwa na maadui, ambao ni Marekani na Israel huku mashirika yao ya intelijensia yakiendesha shughuli zao nyuma ya pazia la harakati zinazofanywa na makundi kama hayo; na akaongeza kwamba, Marekani itakuja kuwajibika kwa mauaji ya watu wa Iraq na hakuna shaka jinai zinazofanywa na utawala huo zitajibiwa tu.

Soko la al Wahilat lililoko kwenye kitongoji cha Sadr mashariki mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, siku ya Jumatatu lilishuhudia mripuko mkubwa wa bomu lililotegwa na genge la kigaidi la DAESH (ISIS) ambao ulisababisha watu wasiopungua 300 kuuawa na wengine 60 kujeruhiwa.

Ijapokuwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh limesambaratishwa nchini Iraq lakini baadhi ya wanachama wake wangaliko maeneo tofauti ya nchi hiyo wakifanya hujuma za kuvizia za kigaidi.../

Tags