-
Video: Daesh wasambaratishwa kikamilifu Iraq, ndoto ya ISIS yayeyuka
Jun 29, 2017 10:52Waziri Mkuu wa Iraq, Haidar al Abadi ametangaza kusambaratishwa dola la uongo la Daesh nchini humo, baada ya vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo kwa kushirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi kukomboa maeneo yote ya Mosul, makao makuu ya mkoa wa Nainawa. Tangazo hilo la Waziri Mkuu wa Iraq limekuja baada ya vikosi vya nchi kuukomboa msikiti mkuu na mkongwe wa al Nuri, katikati ya mji wa Mosul.
-
SAUTI, Makaburi mengine 10 ya halaiki yagunduliwa mkoa wa Kasai Kongo DR, serikali yanyoshewa kidole cha lawama
Jun 27, 2017 11:38Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Pier Numbi ametangaza habari ya kupatikana makaburi mengine 10 ya halaiki katika mkoa wa Kasai nchi humo.
-
SAUTI, Wanachama wa CUF wanaomuunga mkono Profesa Lipumba wamefurahishwa na ufutaji kesi wa jana
Jun 22, 2017 11:46Wafuasi wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, mwenyekiti wa zamani wa chama aliyevuliwa nafasi hiyo na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Hamad, wameonyesha kufurahishwa na uamuzi wa kufuta kesi zote uliofanywa jana.
-
Video na picha mbalimbali za matukio ya mazishi ya Nabra Hassanen aliyeuawa na kijana mwenye chuki za kidini
Jun 22, 2017 10:20Hali ya masikitiko na majonzi yameonekana kutawala mioyo ya maelfu ya Waislamu na wasio Waislamu nchini Marekani tangu kulipotokea mauaji ya binti wa Kiislamu aliyeuawa na kijana mwenye chuki dhidi ya dini ya Uislamu katika jimbo la Virginia nchini humo.
-
Video: Sehemu ya nguvu za makombora za Iran, mara ya kwanza kusambazwa
Jun 21, 2017 05:18Mitandao mbalimbali ya Iran imesambaza kipande cha video kinachoonesha sehemu ya uwezo mkubwa wa makombora wa Iran na jinsi makombora hayo yalivyo na uwezo wa kupiga shabaha kwa umakini na umahiri wa hali ya juu.
-
SAUTI, Viongozi wa Kiislamu Burundi wakosoa tamko la serikali la kutomtambua mke zaidi ya mmoja, wataka marekebisho
Jun 19, 2017 12:36Viongozi wa Kiislamu nchini Burundi wamewataka Waislamu wa nchi hiyo kushikamana na mafundisho ya dini yao hususan katika suala la kuoa zaidi ya mke mmoja ambalo linaonekana kupigwa marufuku na serikali.
-
SAUTI, Muungano wa upinzani nchini Kenya waionya serikali kumkamata kiongozi wake, wasema utamlinda
Jun 19, 2017 12:35Mrengo wa upinzani nchini Kenya umejitokeza na kuishutumu serikali inayoongozwa na muungano wa Jubilee kwa kuendeleza sera za undumakuwili kuhusiana na sakata la matamshi ya kiongozi wake Raila Odinga aliyoyatoa hivi karibuni.
-
VIDEO: Mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya magaidi wa Daesh yameakisiwa kwa wingi duniani
Jun 19, 2017 09:11Mashambulizi ya makombora yaliyofanywa jana usiku (Jumapili) na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH yameakisiwa kwa wingi.
-
Moja ya video zilizochukukliwa na drone za Iran wakati makombora yalipopiga maeneo ya magaidi wa Daesh nchini Syria
Jun 19, 2017 09:05Katika harakati ya kishujaa yenye utaalamu wa hali ya juu, ndege zisizo na rubani za Iran zilikuwa zinapiga picha na kuzituma nchini Iran wakati makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH yalipotua katika maficho ya magaidi wa Daesh.
-
Iran yavurumisha makombora ya balistiki hadi ngome za ISIS nchini Syria+VIDEO
Jun 18, 2017 23:31Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC limetangaza kuvurumisha makombora kadhaa ya balistiki hadi katika ngome ya magaidi wa ISIS katika eneo la Deir Ezzor nchini Syria kama njia ya kuwaadhibu magaidi waliohusika na hujuma za hivi karibuni mjini Tehran.