-
Rais wa Iran aalikwa kuhudhuria mkutano wa BRICS Afrika Kusini
Jul 04, 2023 03:54Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amealikwa rasmi kuhudhuria mkutano ujao wa kundi la BRICS utakaofanyika nchini Afrika Kusini.
-
Mafuriko yauwa watu 7 Afrika Kusini; watu wengine kadhaa hawajulikani walipo
Jun 30, 2023 10:29Mamlaka ya serikali za mitaa nchini Afrika Kusini Ijumaa hii zimetangaza kuwa watu saba wameaga duunia na wengine saba hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko ndani na nje ya mji wa Durban.
-
Rais wa Afrika Kusini anaongoza ujumbe wa viongozi wa Afrika huko Russia na Ukraine
Jun 15, 2023 23:01Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini anaongoza ujumbe wa viongozi wa Kiafrika katika jitihada za kusaka amani huko Ukraine na Russia leo Ijumaa na kesho Jumamosi. Safari hiyo pia ni katika jitihada za kupunguza kile kinachoelezwa kuwa wasiwasi wa nchi za Magharibi kwamba Afrika Kusini inaegemea upande wa Russia katika mzozo wa sasa baina ya Russia na Ukraine licha ya nchi hiyo kukanusha madai hayo.
-
Kasisi wa Kiafrika: Imam Khomeini (RA) alikuwa kiongozi mwenye nguvu na fikra ya kimataifa
Jun 04, 2023 02:49Kasisi wa Afrika Kusini ametangaza kwamba fikra za mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ruhullah Khomeini zilikuwa na taathira kubwa kwa watu na siasa nchini Iran na meneo menginezo ya dunia.
-
Iran na Afrika Kusini zatilia mkazo kustawisha uhusiano baina yao katika nyanja zote
Jun 01, 2023 22:43Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Afrika Kusini wamekutana pambizoni mwa kikao cha kundi la BRICS na kutilia mkazo wajibu wa kustawishwa uhusiano wa pande mbili katika nyanja zote.
-
Amir Abdollahian:Kushiriki katika makongamano ya kimataifa ni moja ya hatua za sera za kigeni za serikali ya Iran
Jun 01, 2023 02:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameutaja ushiriki chanya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika makongamano ya kimataifa kuwa moja ya hatua za doktrini za sera za nje zenye mlingano za serikali ya Iran.
-
Mshukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari Rwanda akamatwa Afrika Kusini
May 25, 2023 21:55Fulgence Kayishema, mmoja kati ya watuhumiwa wakuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 ambaye amekuwa akisakwa kwa udi na uvumba kwa miongo kadhaa sasa hatimaye ametiwa mbaroni nchini Afrika Kusini.
-
Kiongozi wa chama cha EFF cha Afrika Kusini: Russia inapambana na ubeberu, nitaipa silaha
May 24, 2023 08:03Kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), chama cha tatu kwa ukubwa cha kisiasa nchini Afrika Kusini, amesema "ataipatia silaha Russia" katika mzozo wake na Ukraine kwa sababu Moscow iko "katika vita dhidi ya ubeberu".
-
Afrika Kusini yawafurusha wanaotafuta hifadhi waliopiga kambi nje ya ofisi ya UN
Apr 21, 2023 22:09Polisi nchini Afrika Kusini imewafurusha raia wanaotafuta hifadhi zaidi ya 100 waliokuwa wamepiga kambi kwa zaidi ya miaka mitatu nje ya ofisi za Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR mjini Pretoria.
-
Makaburi ya kihistoria ya Waislamu nchini Afrika Kusini yafunguliwa upya baada ya miaka 127
Apr 10, 2023 07:54Makaburi ya kihistoria ya Waislamu yanayopatikana katika barabara ya Brodie huko Wynberg katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini yamefunguliwa tena baada ya kupita miaka 127.