Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetiliana saini makubaliano ya amani na makundi 13 ya waasi ikiwa ni katika juhudi za kuhitimisha vurugu na machafuko yaliyoigubika nchi hiyo na kuhatarisha usalama wa raia.
Kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kimetoa wito wa kusimamishwa haraka iwezekanavyo mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha dhidi ya raia wa nchi hiyo.
Nchi za katikati mwa Afrika na Umoja wa Mataifa zimetoa wito wa kuwepo msukumo na uungaji mkono wa kimataifa kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Umoja wa Mataifa umesema kuna uwezekano jinai dhidi ya binadamu zimefanywa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mapigano yameendelea kushuhudiwa kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo watu 22 wameripotiwa kuuawa.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusiana na wakimbizi ametangaza habari ya kumiminika maelfu ya wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulio ya hivi karibuni ya makundi ya wabeba silaha dhidi ya raia na askari wa kusimamia amani wa umoja huo MINUSCA huko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza kuwa, idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wameingia nchini humo.
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa nchi yake iko tayari kushiriki katika juhudi za kurejesha amani na utulivu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa kuongezeka machafuko na mivutano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kumeifanya hali ya kibinadamu nchini humo kuwa mbaya tangu mwezi Septemba mwaka jana.