Jun 09, 2017 08:07 UTC
  • UN yataka kusitishwa mshambulizi dhidi ya raia huko CAR

Kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kimetoa wito wa kusimamishwa haraka iwezekanavyo mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha dhidi ya raia wa nchi hiyo.

Kikosi hicho cha UN katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kimeashiria katika taarifa yake mashambulizi na ghasia za kikabila na kikaumu zinazoendelea katika miji mingi ya nchi hiyo na kulaani mashambulizi yaliyofanywa kwenye vituo vya kuhifadhi wakimbizi, taasisi za afya na hospitali.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameyatolea mwito makundi yenye silaha kuacha kukwamisha utendaji wa makundi ya misaada ya kibinadamu ya kimataifa na kuyatishia mashirika ya kibinadamu.

Wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati 

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, raia zaidi ya laki moja wamelazimika kuwa wakimbizi katika miezi ya hivi karibuni kufuatia kuibuka ghasia na machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Karibu moja ya tano ya watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakimbizi kufuatia machafuko yaliyoikumba nchi yao na wengine zaidi ya nusu ya jamii ya nchi hiyo wakihitajia misaada ya kibinadamu.

Tags