Mar 16, 2017 14:54 UTC
  • Hali ya kibinadamu Jamhuri ya Afrika ya Kati yazidi kuwa mbaya

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa kuongezeka machafuko na mivutano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kumeifanya hali ya kibinadamu nchini humo kuwa mbaya tangu mwezi Septemba mwaka jana.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo imeashiria kuongezeka machafuko na mivutano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwezi Septemba mwaka jana na katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu na kusisitiza kuwa, raia zaidi ya laki moja wa nchi hiyo wamesajiliwa kama wakimbizi wapya. 

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa, kati ya kila raia watano wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mmoja amekuwa mkimbizi ndani ya nchi au amekimbilia katika nchi jirani kwa ajili ya kupata hifadhi.

Hali halisi inayowakabili wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati 

Idadi ya wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati imefikia laki tisa. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa raia milioni mbili na laki mbili wanahitaji misaada ya kibinadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

 

Tags