Mar 17, 2017 15:40 UTC
  • China: Beijing iko tayari kushiriki katika juhudi za kurejesha amani CAR

Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa nchi yake iko tayari kushiriki katika juhudi za kurejesha amani na utulivu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wuu Haitao ambaye ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amesema katika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo mjini New York kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati imeondoka katika kipindi cha mgogoro na kwamba sasa nchi hiyo imeanza ukurasa mpya.

Nusu ya jamii ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati inahitaji msaada wa haraka wa chakula.

Nchi hiyo ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani mwaka 2013 baada ya kuibuka mapigano ya kikabila na kupinduliwa serikali iliyokuwepo madarakani. Mapigano hayo yalisababisha ukosefu mkubwa wa amani na kuwalazimisha maelfu ya raia wa nchi hiyo kuwa wakimbizi ndani ya nchi na katika nchi jirani.

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopo nchini humo pia kimeshindwa kuzuia hali hiyo ya ukosefu wa amani na mauaji ya raia. 

Wanawake wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati 

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeashiria kuongezeka machafuko na mivutano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwezi Septemba mwaka jana na katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu na kusisitiza kuwa, raia zaidi ya laki moja wa nchi hiyo wamesajiliwa kama wakimbizi wapya. 

Tags