Sep 22, 2024 02:58 UTC
  • China yakosoa na kulaani jinai za Israel nchini Lebanon

Mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, mashambulizi ya kikatili, ya kutisha na yasiyo na mfano ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon ni ukiukaji mkubwa wa mamlaka ya nchi huru, sheria za kimataifa na za kibinadamu.

Fu Cong, balozi na mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amesema hayo katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama ulioitishwa kwa ajili ya kujadili mashambulizi ya mauaji ya umati ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Lebanon na hatari ya kuenea kwa migogoro katika eneo na kubainisha kuwa, watoto, wanawake, madaktari na wengi wao wakiwa raia walilengwa katika mashambulizi ya utawala wa Israel.

Mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, wahusika na watenda wa jinai hizo lazima wawajibishwe.

Fu Cong amekkosoa na kulaani vikali jinai za Israel huko Lebanon na kutoa mwito wa kuchukuliqwa hatua za kukomesha jinaii za utawala huo ghasibu dhiidi ya raia.

 

Mapema siku ya Ijumaa, utawala wa  Israel ulitekeleza hujuma katika mji wa  Beirut na kuua takriban watu 14 na kujeruhi wengine 66.

Kulingana na Shirika rasmi la Habari la Kitaifa la Lebanon (NNA), watoto watano ni miongoni mwa waliouawa katika hujuma hiyo ya kigaidi ya Israel.

Kanali ya televisheni ya al-Mayadeen ya Lebanon imesema ndege isiyo na rubani ilivurumishha makombora kadhaa katika kitongoji cha Dahiyeh chenye wakazi wengi mjini Beirut. Nalo Shirika rasmi la Habari la Kitaifa la Lebanon limesema ndege ya kivita aina ya F35 ilitumika katika hujuma hiyo.

 Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imethibitisha kuuawa kamanda wake wa ngazi ya juu Ibrahim Aqil katika hujuma hiyo ya kigaidi iliyotekelezwa utawala haramu wa Israel jijini Beirut.

Tags