Oct 07, 2024 02:41 UTC
  • Hizbullah; imara zaidi kuliko wakati wowote

Ni matumaini yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi hiki maalumu ambacho kitazungumzia jinsi Hizbullah ya Lebanon ilivyokuwa imara na madhubuti hii leo kuliko wakati mwingine wowote.

Kipindi hiki kinachokujieni kwa mnasaba wa maombolezo ya kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon. Kuweni nami hadi mwisho wa kipindi hiki.

Lau vikosi vya muqawama vya Palestina kama vile Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Jihadul Islami na watu wengine wenye ghera na uchungu na ardhi ya Palestina hawangekuwepo, Wazayuni makatili wasingembakisha hata Mpalestina mmoja akiwa hai hadi sasa. Hao ndio ambao wameilinda Palestina kwa miaka mingi. Wapalestina wanafuundishwa utamaduni wa kujitolea mhanga na kuuawa shahidi tangu wakiwa katika kipindi cha utoto wao na hujifunza muqawama na kusimama kidete kuanzia kipindi hicho hicho cha utoto wao. Quran inatupa bishara  kwa kutwambia kwamba, muqawama na kusima kidete ndio siri ya ushindi mkubwa. Aya ya 30 ya Surat Fussilat inasema:

Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa (yaani wakasimama kidete), hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa.

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, chini ya bendera ya Imam Khomeini, yalipata ushindi kwa ustahimilivu na kusimama kidete katika njia ya haki na kuwa tumaini la wapigania uhuru ulimwenguni. Kusimama kidete na kutotetereka katika haki, ni mithili ya dirisha la nuru ambalo huangazia giza na huisukuma kando na kuifanya nafasi iwe angavu na yenye matumaini.

 

Hizbullah ya Lebanon pia iliundwa na muqawama wa waumini na wanamapinduzi; Wakati Lebanon ilipokuwa inaelekea kufa kutokana na mashinikizo ya Wazayuni, kwa juhudi za kijasiri za Imam Musa Sadr, Sayyid Abbas Mousavi, Mostafa Chamran na mwanafunzi wao kijana Sayyid Hassan Nasrullah, kundi la Mujahidina lililopewa jina la "Hizbullah" liliundwa. Ndani ya harakati hiyo, walilelewa vijana wenye hima, bidii na ghera ya ardhi na dini yao ambao mpaka leo wangali wanautikisa mwili wa mbwa mwitu wa Kizayuni yaani utawala ghasibu wa Israel.

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon iliasisiwa mwaka 1982 kwa shabaha ya kukabiliana na utawala haramu wa Israel. Harakati hii iliasisiwa kwa himaya na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hizbullah ilianzisha harakati zake dhidi ya Israel kwa operesheni za kujitolea kufa kishahidi. Kisha baadaye ikaongeza nguvu zake za kijeshi na ikawa ikikabiliana na Israel kwa makombora ya Katyusha na vita vya msituni.

Katibu Mkuu wa kwanza wa Hizbullah ya Lebanon alikuwa Subhi Tufayli ambaye alichaguliwa kushika wadhifa huo tarehe 2, Novemba 1989. Kabla ya hapo, kwa muda wa miaka saba chama hicho kilikuwa kikiongozwa kwa mtindo wa Baraza la Uongozi. Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah, Subhi Tufayli, Sayyid Abbas Musawi, Sayyid Hassan Nasrullah, Sheikh Naim Qassim, Hussein Kurani, Hussein Khalil, Muhammad Raad, Muhammad Fneish, Muhammad Yazbek na Ibrahim Amin ni miongoni mwa waliokuwa waasisi wa Hizbullah ya Lebanon.

Mei 1991 Sayyid Abbas Musawi akachaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Hizbullah.

Sayyid Abbas Musawi, Katibu Mkuu wa zamani Hizbullah

 

Katika kipindi cha uhai wake Sayyid Abbas Musawi alitumia muda wake mwingi akiwa pamoja na Wapalestina kuendesha mapambano dhidi ya Israel. Harakati ya Hizbullah ya Lebanon mwaka 1985 ilitangaza rasmi itikadi na stratejia yake ya kukabiliana na Israel. Harakati za Hizbullah katika miaka ya awali ya kuasisiwa kwake zilijikita zaidi katika operesheni za kujitolea kufa shahidi dhidi ya wanajeshi wa Israel; lakini hatua kwa hatua mbinu hii ikabadilika.

Tarehe 16 Februari 1992 Sayyid Abbas Musawi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon, aliuawa shahidi katika shambulio la ndege za utawala wa Kizayuni wa Israel huko kusini mwa nchi hiyo. Shambulio hilo lilipelekea kuuawa pia watu kadhaa waliokuwa wameandamana naye akiwemo mke na mwanawe mdogo, pamoja na wasaidizi wake watatu. Shambulio hilo lilitokea wakati Sayyid Abbas Musawi alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwenye kumbukumbu za kuuawa shahidi Sheikh Raghib Harb aliyeuliwa na maafisa wa utawala huo miaka michache iliyopita kabla ya hapo. Baada ya kuuawa shahidi Sayyid Abbas Musawi, Sayyid Hassan Nasrullah alichukua jukumu la kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, na kutoa pigo kwa Israel mwaka 2000, baada ya kuyafukuza kwa madhila majeshi ya utawala huo katika ardhi za kusini mwa Lebanon.

Katika kipindi cha uongozi wake akiwa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebaanon, Shahidi Sayyid Nasrullah ameacha mafanikio makubwa katika faili la utendaji wake katika uuga wa kisiasa na kijeshi.

Hizbullah ilishiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa Lebanon mwaka 1992 na kufanikiwa kupata viti vinane na miaka iliyofuata viti hivyo viliongezeka na kuuifanyya harakati hiyo kuzidi kuuwa na nguvuu katika siasa za Lebanon.

 

Licha ya kuwa, Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imejikita zaidi katika suala la muqawama na kupambana na hujuma na uvamizi wa Israe; lakini pamoja na hayo, chama hiki kinafanya pia harakati mbalimbali za kijamii na imefanikiwa pakubwa pia katika uga huo na miongoni mwa mafanikio hayo ni kuanzisha taasisi za jihadi ya ujenzi kwa ajili ya kukarabati maeneo yaliyoharibiwa na hujuma na mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel na majanga ya kimaumbile kama mafuriko, tetemeko la ardhi na kadhalika.

Hii leo licha ya upinzani mkubwa wa madola ya kibeberu kwa Hizbullah na hata baadhi ya mataifa kuiweka harakati hii katika orodha ya eti makundi ya kigaidi, Hizbullah ina wafuasi na waungaji mkono wengi duniani. Mataifa muhimu yanayoiunga mkono Hizbullah ni Iran na Syria. Russia pia inaihesabu Hizbullah kama harakati halali ya kisiasa nakijamii. Hii leo Hizbullah imeimarika na kupata nguvu zaidi kuliko wakati wowote na inahesabiwa kuwa nguvu muhimuu mno katika eneo la Asia Magharibi na imekuwa mwiba katika koo la Israel ambayo kwa kuweko Hizbullah imeshindwa kufikia malengo yake haramu huusuusan nchini Lebanon.

Wapenzi wasikilizaji muda wa kipindi chetu kwa leo uumefikia tamati, ambapo leo kwa muktasari kilizungumzia harakati ya Hizbullah na jinsi harakati hii ilivyoimarika na kupata mafanikio kuliko wakati wowote. Basi hadi tutakapokutana tena wakati mwingine ninakuageni nikikutakieni kila la kheri.

Tags