Oct 05, 2024 06:01 UTC
  • Hizbullah yavurumisha makombora kwenye maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel

Duru za habari zimeripoti kuwa, makombora na maroketi 70 yamerushwa kutoka Lebanon kuelekea kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Gazeti la Kizayuni la Yediot Aharnot limetangaza kuwa, makombora na maroketi 70 yalirushwa kutoka kusini mwa Lebanon siku ya Ijumaa jioni  katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Vyombo vya habari pia vimeripoti kuhusu moto unaoenea katika milima ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na Israel  na karibu na makazi ya Wazayuni ya Kiryat Shmona.

Tangu Ijumaa asubuhi, ving'ora vya tahadhari vimekuwa vikisikika katika maeneo mengi ya kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni.

Tangu jana Ijumaa, wanamapambano wa Lebanon wamefanya oparesheni 23 dhidi ya maeneo ya utawala wa Kizayuni huko kaskazini mwa Palestina na maeneo ya mpakani mwa Lebanon.

Jeshi katili  la Kizayuni, ambalo limekuwa likipokea vipigo vikali kutoka kwa Hizbullah ya Lebanon tangu tarehe 8 Oktoba, linawalenga kwa makusudi raia wa kusini mwa nchi hiyo ili kufidia kushindwa kwake katika medani ya vita.

Hizbullah inakabiliana na jinai hiyo ya Wazayuni kwa kushadidisha mashambulizi yake dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na pia kushambulia vituo vya kijeshi vya  Wazayuni katika eneo hilo.