Pars Today
Raia wasiopungua 10, wakiwemo watoto watatu, wameuawa katika hujuma ya pamoja na Jeshi la Marekani na Jeshi la Somalia kusini mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Serikali ya Somalia imetangaza habari ya kuuawa watu 10 ambao ni raia wa kawaida katika shambulizi la wabeba silaha kijiji cha Barire, jimbo la Lower Shebelle, kusini mwa nchi hiyo.
Kwa akali watu watatu wameuawa kwa kukatwa vichwa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabab katika kaunti ya Lamu, pwani ya Kenya.
Kaimu Mkuu wa zamani wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al Shabab lenye makao yake huko Somalia amewataka wanamgambo wa kundi hilo wajiengue kundini kufuatia hatua ya kiongozi huyo kujiunga na serikali ya Mogadishu hivi karibuni.
Serikali ya Somalia imayaonya mashirika na taasisi za mawasiliano na za kifedha zinazohusika na usafirishaji wa fedha kwa ajili ya kundi la kigaidi na kiwahabi la al Shabab nchini humo.
Aliyekuwa Naibu Kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab na pia msemaji wa zamani wa genge hilo la ukufurishaji Mukhtar Robow Abu Mansur, amejisalimisha kwa jeshi la nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Ndege za Jeshi la Ulinzi la Kenya KDF zimeshambulia ngome za kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab katika eneo la Weelmarow karibu na wilaya ya Afmadow, eneo la Lower Juba, kusini mwa Somalia.
Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab la Somalia limetangaza kuwa limeuteka na kuudhibiti mji wa Leego, ulioko kusini mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Huku uchaguzi mkuu wa Agosti 8 ukizidi kujongea nchini Kenya, kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab linaonekana kushadidisha mashambulizi yake dhidi ya raia na maafisa usalama wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Wizara ya Habari ya Somalia imetangaza kuwa kiongozi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la ash-Shabab anayehusika na suala la kupanga shambulizi ya kundi hilo ameangamizwa la jeshi la nchi hiyo.