Pars Today
Jeshi la Somalia katika operesheni ya pamoja na kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM limefanikiwa kuharibu kituo kimoja kikubwa cha magaidi wa as-Shabaab kusini mwa nchi hiyo.
Wapiganaji wasiopungua 18 wa kundi la kigaidi la al Shabab wameuawa katika operesheni iliyofanywa na jeshi la Somalia katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Watu wanaodhaniwa kuwa magaidi wa kundi la la Shabab wamewachinja kwa kuwakata vichwa watu 9 katika shambulizi lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika kijiji kimoja cha Kaunti ya Lamu huko pwani mwa Kenya.
Maafisa wawili wa polisi nchini Kenya wameuawa baada ya magaidi wanaoaminika kuwa wa kundi la Al Shabab kushambulia kituo cha polisi katika eneo la Pandanguo katika Kaunti ya Lamu.
Ripoti zinasema kuwa, kumetokea hitilafu na mgawanyiko katika kundi la kigaidi la al Shabab la Somalia baada ya kusambaa habari kwamba, msemaji wa kundi hilo amejitenga na kwamba anaungwa mkono na jeshi la serikali ya Mogadishu.
Viongozi wa kijeshi katika eneo la Puntland, kaskazini mwa Somalia, wamewanyonga wanachama saba wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la ash-Shabab.
Vikosi vya usalama vya Somalia vimewaua wapiganaji sita wa kundi la kigaid na kitakfiri la al-Shabab na kujeruhiwa makumi ya wengine.
Watu watano wanaripotiwa kuuawa nchini Kenya katika mji wa El Wak kaunti ya Mandera eneo la kaskazini mashariki kufuatia hujuma ya kundi la kigaidi la al-Shabab.
Watu wasiopungua 15 wameuawa katika hujuma ya kigaidi huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia huku kundi la kigaidi la al-Shabab likitangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Askari wa serikali ya Somalia amehukumiwa kifo kwa kumuua waziri wa serikali ya Mogadishu baada ya kudhania kuwa ni mmoja kati ya wanachama wa kundi ya kigaidi la al Shabab.