Wapiganaji 18 wa Al Shabab wauawa kaskazini mwa Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31572-wapiganaji_18_wa_al_shabab_wauawa_kaskazini_mwa_somalia
Wapiganaji wasiopungua 18 wa kundi la kigaidi la al Shabab wameuawa katika operesheni iliyofanywa na jeshi la Somalia katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 10, 2017 01:53 UTC
  • Wapiganaji 18 wa Al Shabab wauawa kaskazini mwa Somalia

Wapiganaji wasiopungua 18 wa kundi la kigaidi la al Shabab wameuawa katika operesheni iliyofanywa na jeshi la Somalia katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Kanali Muhammed Ismail ambaye ni miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Somalia amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo mapema leo limeshambulia ngome ya al Shabab katika eneo la Bilad Bent na kuua wanachama 18 wa kundi hilo.

Duru za kijeshi la Somalia zinasema kuwa, operesheni ya jeshi hilo ya kuwasaka wapiganaji wa kundi la al Shabab huko kaskazini mwa nchi hiyo imeharibu ngome na vituo kadhaa vya kundi hilo. 

Wapiganaji wa al Shabab wauawa Somalia

Kundi la al Shabab limekiri kwamba, limeshambuliwa na jeshi la serikali ya Somalia lakini limekanusha ripoti za kuuawa wapiganaji wake.

Kundi hilo la kigaidi lingali linadhibiti baadhi ya maeneo ya Somalia na limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kujilipua kwa mabomu nchini humo na katika nchi jirani ya Kenya.