Kuharibiwa kituo cha as-Shabaab kusini mwa Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32100-kuharibiwa_kituo_cha_as_shabaab_kusini_mwa_somalia
Jeshi la Somalia katika operesheni ya pamoja na kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM limefanikiwa kuharibu kituo kimoja kikubwa cha magaidi wa as-Shabaab kusini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 22, 2017 02:23 UTC
  • Kuharibiwa kituo cha as-Shabaab kusini mwa Somalia

Jeshi la Somalia katika operesheni ya pamoja na kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM limefanikiwa kuharibu kituo kimoja kikubwa cha magaidi wa as-Shabaab kusini mwa nchi hiyo.

Operesheni hiyo ilitetekelezwa kwa mafanaikio jana Ijumaa katika eneo la Toro Toro kusini mwa Somalia ambapo kituo kikubwa cha as-Shabaab katika eneo hilo kimeharibiwa kabisa. Kikosi cha AMISOM kimetoa taarifa mjini Mogadishu kikisema kuwa kuharibiwa kwa kituo hicho muhimu kwa as-Shabaab bila shaka kutapunguza pakubwa uwezo wa wanamgambo hao wa kutekeleza hujuma za kigaidi dhidi ya raia wa Somalia.

Sehemu ya uharibifu unaofanywa na as-Shabaab nchini Somalia

Kundi hilo la kigaidi ambalo limefurushwa kutoka  miji mikubwa ya nchi hiyo, na hasa Magadishu mji mkuu, limezidisha mashambulio yake ya kigaidi dhidi ya jeshi na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM. Somalia ambayo inahesabiwa kuwa moja ya nchi masikizi zaidi duniani imekuwa ikikabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tokea mwaka 1991 kipindi ambacho ambapo Siad Barre aliyekuwa rais wa nchi hiyo alingólewa madarakani.