Askari wa Somalia aliyemuua waziri ahukumiwa kifo
(last modified Mon, 19 Jun 2017 15:30:50 GMT )
Jun 19, 2017 15:30 UTC
  • Askari wa Somalia aliyemuua waziri ahukumiwa kifo

Askari wa serikali ya Somalia amehukumiwa kifo kwa kumuua waziri wa serikali ya Mogadishu baada ya kudhania kuwa ni mmoja kati ya wanachama wa kundi ya kigaidi la al Shabab.

Afisa wa jeshi la Somalia, Hassan Ali Noor amesema kuwa, Mahakama ya Kijeshi ya nchi hiyo imemhukumu kifo askari Ahmed Abdulahi Ahmed kwa kumpiga risasi na kumuua kimakosa waziri wa serikali.

Abbas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa waziri wa kazi za umma wa serikali ya Somalia alipigwa risasi akiwa katika gari lake mjini Mogadishu mapema mwezi Mei.

Siraji aliyekuwa na umri wa miaka 31 alikulia katika kambi ya wakimbizi wa Kisomali nchini Kenya na alikuwa waziri mwenye umri mdogo zaidi katika serikali ya Somalia.

Wapiganaji wa kundi lakigaidi la al Shabab

Magaidi wa kundi la al Shabab wamekuwa wakishambulia viongozi na ofisi za serikali ya Somalia na taasisi za kimataifa nchini Somalia na katika nchi kama Kenya na Uganda.   

Tags