Mgawanyiko waripotiwa katika safu za al Shabab, Somalia
(last modified Sun, 02 Jul 2017 06:13:17 GMT )
Jul 02, 2017 06:13 UTC
  • Mgawanyiko waripotiwa katika safu za al Shabab, Somalia

Ripoti zinasema kuwa, kumetokea hitilafu na mgawanyiko katika kundi la kigaidi la al Shabab la Somalia baada ya kusambaa habari kwamba, msemaji wa kundi hilo amejitenga na kwamba anaungwa mkono na jeshi la serikali ya Mogadishu.

Habari zinasema, Mukhtar Robow Abu Mansur ambaye alikuwa msemaji wa kundi la al Shabab na naibu kiongozi wa kundi hilo la kigaidi amebadili misimamo yake na kuamua kufanya mazungumzo na serikali ya Somalia.

Habari za ndani zinasema, Robow alianza mchakato wa kujitenga na kundi la al Shabab mwaka 2013 na kwamba amekuwa akiendesha mchakato huo kwa siri. 

Hadi sasa maafisa wa jeshi la Somalia hawajathibitisha habari ya kusalimu amri Mukhtar Robow Abu Mansur.

Robow Abu Mansour (kushoto)

Kundi la kigaidi la al Shabab lingali linadhibiti maeneo machache ya kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa Kenya na limekuwa likiendesha shughuli zake kupitia mashambulizi ya kujilipua kwa mabomu.     

Tags