-
Vita baina ya Marekani na Canada sasa vyaingia michezoni; wimbo wa taifa wa Marekani wazomewa
Feb 03, 2025 10:31Mashabiki wa michezo wa Canada wamekuwa wakizomea wimbo wa taifa wa Marekani kila unapopigwa katika mechi mbalimbali ikiwa ni kuonesha hasira zao kwa amri ya rais wa Marekani Donald Trump ya kutozwa ushuru mkubwa bidhaa zinazoingizwa Marekani kutokea Canada.
-
Jeshi la Tanzania lathibitisha kuuwa askari wake wawili DRC, Rwanda yakaribisha kujadiliwa mzozo
Feb 03, 2025 05:53Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza kuwa, wanajeshi wake wawili ni miongoni mwa askari 20 wa kulinda amani waliouawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Ushuru wa Trump: Canada na Mexico zajibu mapigo, China yaonya
Feb 03, 2025 02:27Canada, Mexico na China zimeapa kujibu mapigo ya uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani, wa kutoza ushuru wa juu kwa mataifa hayo matatu, na kuisukuma Washington katika vita vya kibiashara na nchi mbili jirani, na China yenye nguvu kubwa.
-
Wamisri wakusanyika mbele ya Kivuko cha Rafah, wakipinga kuhamishwa Wapalestina wa Gaza
Feb 01, 2025 02:31Raia wa Misri walikusanyika jana Ijumaa mbele ya kivuko cha mpakani cha Rafah na Ukanda wa Gaza wakipinga pendekezo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kuwafukuza Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza na kuwapeleka nje ya nchi yao.
-
Uhuru wa kujieleza kwa mtindo wa Trump; Wanafunzi wa Marekani wanaounga mkono Palestina wanafukuzwa
Jan 31, 2025 02:52Rais wa Marekani ametia saini amri ya kufuatilia shughuli za wanafunzi wa vyuo vikuu na kuwafukuza iwapo itagundulika kuwa wanaiunga mkono Palestina!
-
Trump ang'ang'ania mpango wake wa kutaka Wapalestina wahamishwe Ghaza, amwalika Netanyahu
Jan 29, 2025 03:28Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kung'ang'ania pendekezo lake la kuhamishwa Wapalestina wote katika Ukanda wa Ghaza, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Huduma mpya za Trump kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Jan 29, 2025 02:35Katika siku za mwanzo za muhula wake wa pili wa uongozi, Donald Trump, rais mpya wa Marekani, kwa mara nyingine tena amefuata njia ile ile aliyopitia katika muhula wa kwanza wa uongozi wake. Katika muhula wa kwanza, Trump alitoa uungaji mkono mkubwa na ambao haujashuhudiwa kwa utawala wa Kizayuni na kuchukua hatua mpya sambamba na kuiunga mkono Israel na kuwapinga Wapalestina. Vitendo na misimamo hii imekutana na majibu chanya kutoka Tel Aviv.
-
Kwa nini Trump hastahamili kuwepo kwa wahamiaji Waislamu huko Marekani?
Jan 28, 2025 02:53Moja ya amri tisa za Donald Trump katika siku ya kwanza ya uongozi wake ni kupitiwa upya sheria ya kurejesha marufuku ya Waislamu kuingia Marekani, suala ambalo iwapo litaidhinishwa na kutekelezwa, litakuwa na madhara makubwa kwa wahamiaji Waislamu nchini Marekani na hata waombaji visa Waislamu.
-
Rais wa Colombia alegeza kamba baada ya Trump kuamuru vikwazo dhidi ya nchi hiyo
Jan 27, 2025 07:14Rais Donald Trump wa Marekani jana alisema kuwa ataiwekea Colombia ushuru wa asilimia 25 na vikwazo baada ya nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kukataa kuruhusu kutua nchini humo ndege mbili za kijeshi za Marekani zilizobeba wahamiaji waliofukuzwa huko Marekani.
-
Uroho wa Trump katika muhula wa pili wa urais wake
Jan 27, 2025 04:41Rais Donald Trump wa Marekani ameanza muhula wake wa pili wa uongozi huku akiweka hadharani uroho wake wa kupora ardhi, biashara na fedha za mataifa mengine ambapo ametangaza wazi azma yake ya kutaka kunyakua na kuunganisha ardhi za nchi huru na Marekani na pia kuhodhi kandarasi zenye faida kubwa kutoka kwa washirika wa Washington.