-
Uchaguzi wa rais wa 2020; nembo ya demokrasia bandia ya Marekani
Nov 07, 2020 06:44Kama ilivyokuwa imetabiriwa awali, uchaguzi wa mwaka huu wa rais wa Marekani ambao ulifanyika tarehe 3 mwezi huu wa Novemba umekuwa moja ya chaguzi zenye utata mkubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo, uchaguzi ambao taathriza zake bila shaka zitabakia kwa muda mrefu katika uwanja wa siasa za nchi hiyo.
-
Wafuasi wa Trump wenye bunduki wazingira vituo vya kuhesabu kura
Nov 07, 2020 04:09Idadi kubwa ya wafuasi wa Rais Donald Trump wa Marekani wameonekana katika vituo kadhaa vya kuhesabu kura nchini humo wakiwa wamebeba bunduki za rashasha.
-
Wademocrati waanza kusherehekea ushindi, Biden akaribia zaidi White House
Nov 06, 2020 23:55Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden anaendelea kumtimulia kivumbi mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump katika matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani kwenye majimbo mawili muhimu ya Pennsylvania na Georgia ambayo huenda yakamkabidhi rasmi Biden ufunguo wa kuingia Ikulu ya White House.
-
Mpwa wa Trump: Hali Marekani itakuwa hatari sana miezi inayokuja
Nov 06, 2020 08:09Mpwa wake rais wa Marekani Donald Trump ametahadharisha kuwa, hali nchini Marekani itakuwa hatari sana katika miezi ijayo kwa sababu Trump hatakubali kushindwa katika uchaguzi.
-
Kujiondoa rasmi Marekani katika Mapatano ya Tabianchi ya Paris
Nov 05, 2020 04:22Marekani ambayo imejiondoa katika mikataba kadhaa ya kimataifa wakati wa utawala wa Donald Trump, sasa imejiondoa rasmi katika Makubaliano ya Mabadiliko ya Tabianchi yaliyofikiwa mjini Paris, Ufaransa mwaka 2015. Mapatano hayo ni muhimu katika kulinda mazingira ili kuzuia ongezeko la joto duniani.
-
Kurefusha Marekani vikwazo dhidi ya Sudan; zawadi ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel
Nov 03, 2020 10:11Serikali ya Trump ikiwa na lengo la kuuridhisha utawala wa haramu wa Israel imechukua hatua tofauti ikiwemo ya kuandaa uwanja wa kutambuliwa rasmi utawala huo na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu ambapo hatua yake ya karibuni kabisa na kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Sudan na utawala huo ghasibu.
-
Mkuu wa zamani wa CIA: Nina wasiwasi wa Trump kujitangaza mshindi mapema
Nov 02, 2020 09:56Mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani CIA amesema, ana wasiwasi wa machafuko ya uchaguzi na rais wa nchi hiyo Donald Trump kujitangaza mshindi wa uchaguzi mapema.
-
Kushadidi migawanyiko ya kisiasa na kijamii Marekani
Nov 02, 2020 08:08Kampeni za uchaguzi wa rais wa Marekani zimefika ukingoni. Ikiwa imesalia masaa machache kabla ya uchaguzi mkuu, kumeshuhudiwa majibizano makali baina ya wagombea urais na wafuasi wao na hata katika baadhi ya maeneo kumeripotiwa kuongezeka mapigano ya mitaani baina ya wafuasi wa kambi mbili hasimu za kisiasa.
-
'Trump ni gaidi nambari moja duniani'
Oct 31, 2020 23:18Mshauri wa sera za kigeni wa Spika wa Bunge la Iran ameashiria mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye aliuawa kigaidi kufuatia amri ya Rais Donald Trump wa Marekani na kusema, Trump ni gaidi nambari moja duniani.
-
Sanders: Donald Trump ana maradhi ya kusema uongo na fikra za kidikteta
Oct 31, 2020 07:34Seneta wa jimbo la Vermont na mwanasiasa mashuhuri wa Marekani, Bernie Sanders amemtaja Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuwa ni kidhabi, na kusisitiza kuwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 3 Novemba mwaka huu nchini humo ndio muhimu zaidi katika historia ya Marekani.