-
Amnesty: Jeshi la Eritrea linaendelea kuua raia Tigray, Ethiopia
Apr 15, 2021 23:04Shirika la kutetea haki za binadamu la Amesty International limesema jeshi la Eritrea lingali linaua raia katika eneo la Tigray, wiki chache baada ya Ethiopia kutangaza kuwa wanajeshi wa nchi hiyo jirani yake wameanza kuondoka katika eneo hilo linalokumbwa na mgogoro na mapigano kwa miezi kadhaa sasa.
-
Ethiopia inakabiliwa na uhaba wa mitungi ya oxygen kwa ajili ya wagonjwa wa corona
Apr 13, 2021 07:26Moja ya viwanda vikubwa vya kutengeneza oxygen nchini Ethiopia ambavyo kwa siku hudhamini zaidi ya mitungi elfu mbili ya hewa ya oxygen kwa ajili ya wagongwa wa corona nchini humo kimekumbwa na matatizo ya kiufundi.
-
Sudan: Hakuna ufumbuzi wa kijeshi wa mgogoro wa bwawa la Renaissance
Apr 09, 2021 08:57Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Sudan amesema kuwa, ni jambo lililo mbali kwamba mgogoro wa bwawa la Renaissance unaweza kutatuliwa kwa njia za kijeshi ili kuizuia Ethiopia kuendeleza mradi ujenzi wa bwawa hilo juu ya maji ya Mto Nile.
-
Kushindwa mara kadhaa mazungumzo kuhusu bwawa la An Nahdhah; Misri yatoa vitisho
Apr 08, 2021 22:08Mazungumzo ya kuainisha suala la maji ya bwawa la An Nahdhah na kuanza marhala ya pili ya uingizaji maji bwawani kwa mara nyingine tena yamegonga mwamba; na kumalizika bila ya natija yoyote huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Baada ya kufeli mazungumzo hayo, Misri imeitishia Ethiopia kwamba itachukua hatua.
-
Rais wa Misri aonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita na Ethiopia
Apr 08, 2021 03:08Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri ameionya Ethiopia kuhusu kutokea vita baina ya nchi hizo mbili iwapo Addis Ababa itaendelea kushikilia msimamo wake wa kuingiza maji katika bwawa la al Nahdha.
-
Wafugaji 100 wauawa katika mapigano ya kugombania ardhi Ethiopia
Apr 07, 2021 03:15Mapigano baina ya wafugaji wa jamii hasimu zinazopakana katika eneo la Afar na Somali kaskazini mashariki mwa Ethiopia yamepelekea watu zaidi ya 100 kuuawa.
-
Ethiopia yaalani taarifa ya kundi la G-7 kuhusu eneo la Tigray
Apr 06, 2021 22:31Ethiopia imelaani na kukosoa taarifa iliyotolewa katika kikao cha kundi la G-7 kuhusu hali ya mambo katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Kivuko cha mpakani kati ya Sudan na Ethiopia chafungwa
Apr 05, 2021 00:03Viongozi wa Sudan wamechukua uamuzi wa kukifunga kivuko cha mpakani kati ya nchi hiyo na Ethiopia.
-
Watu 30 wauliwa katika shambulizi la silaha, nchini Ethiopia
Apr 01, 2021 03:46Watu waliokuwa na bunduki wamewauwa raia wasiopungua 30 katika shambulio lililolenga kijiji kimoja katika mkoa wa Oromia nchini Ethiopia. Shambulizi hilo linatambuliwa kuwa ni katika mfululizo wa ghasia za kikabila za hivi karibuni za wapinzani wa serikali ya shirikisho.
-
Al Sisi aionya Ethiopia, asema maji ya Misri na mstari mwekundu, anayetaka kujaribu atakiona..
Mar 30, 2021 22:35Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri ametishia kutoa jibu lisilotasawarika iwapo nchi yake itapata madhara kutokana na bwana la Renaissance linalojengwa na Ethiopia juu ya maji ya Mto Nile.