-
Imarati yamtimua balozi wake wa Ethiopia kwa kushindwa kuandaa safari ya mkuu wake
Apr 20, 2018 09:38Serikali ya Imarati imemrejesha nyumba na kumpiga kalamu nyekundu balozi wake nchini Ethiopia.
-
Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia alifanyia mabadiliko baraza la mawaziri ili kutekeleza mageuzi
Apr 19, 2018 23:46Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia Abiy Ahmed ameteua waziri mpya wa ulinzi ikiwa ni sehemu ya mabadiliko aliyofanya katika serikali yake ili kusaidia kutekeleza mageuzi yaliyokuwa yakipiganiwa na wananchi wakati wa maandamano ya machafuko ambapo mamia ya watu waliuliwa na askari wa usalama wa nchi hiyo.
-
Maelfu ya watu wakimbia makazi yao Ethiopia
Apr 16, 2018 09:50Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao katika maeneo ya mpaka wa Ethiopia na Somalia kutokana na mapigano makali yanayoendelea katika eneo hilo.
-
Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia auzuru mji uliokuwa kitovu cha maandamano dhidi ya serikali
Apr 11, 2018 22:04Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia jana Jumatano aliahidi kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoukabili mkoa anakotoka wa Oromo; ambao umekuwa kitovu cha machafuko makubwa yaliyotishia uhai wa muungano wa chama tawala nchini Ethiopia.
-
Misri, Sudan na Ethiopia zashindwa kuafikiana kuhusu bwawa la al-Nahdha
Apr 06, 2018 09:50Mkutano wa Misri, Sudan na Ethiopia wa kujadili suala tata la bwawa la al-Nahdha umegonga mwamba huku pande tatu hizo zikishindwa kuafikiana.
-
Hatimae Abiy Ahmed Ali awa rasmi waziri mkuu wa Ethiopia
Apr 02, 2018 21:54Abiy Ahmed Ali aliyekuwa anakaimu nafasi ya waziri mkuu wa Ethiopia baada ya maandamano ya wananchi kumlazimisha kujiuzulu waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Hailemariam Desalegn, jana Jumatatu aliapishwa kuwa waziri mkuu rasmi wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Zaidi ya watu 1000 watiwa mbaroni nchini Ethiopia
Mar 31, 2018 23:42Watu elfu moja na 107 wametiwa mbaroni nchini Ethiopia kwa tuhuma za kuvunja sheria za hali ya hatari nchini humo.
-
Ethiopia kumwapisha Waziri Mkuu mpya Aprili Pili
Mar 30, 2018 03:42Waziri Mkuu mteule wa Ethiopia, Abiye Ahmed ataapishwa Jumatatu ijayo. Hayo yameelezwa na Bunge la Ethiopia baada ya muungano wa chama tawala kumchagua kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa na Hailemariam Desalegn, Waziri Mkuu wa Ethiopia aliyejiuzulu.
-
UNHCR: Waethiopia waliokimbilia hifadhi Kenya wakumbwa na masaibu
Mar 29, 2018 02:01Maelfu ya wakimbizi wa Ethiopia waliokimbilia hifadhi nchi jirani ya Kenya hivi sasa wanakabiliwa na tatizo kubwa la kukidhi mahitaji yao ya msingi, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.
-
Ethiopia yaituhumu Eritrea kuwa inataka kuvuruga usalama wake
Mar 18, 2018 23:46Ethiopia imemtuhumu jirani yake Eritrea kuwa inataka kuvuruga usalama wake kwa kuyaunga mkono yale iliyoyaita makundi "haribifu" katika kipindi hiki ambapo sheria ya hali ya hatari inatekelezwa nchini humo.