Pars Today
Harakati ya Wananchi ya al Hashdu sh-Sha'abi nchini Iraq imefanya shambulizi dhidi ya ngome na maeneo ya magaidi wa kundi la Daesh (ISIS) katika mkoa wa Deir ez-Zor nchini Syria, ambapo kwa akali magaidi 15 wameangamizwa.
Maafisa usalama wa Misri wametangaza habari ya kuuawa magaidi 14 katika mkoa wa Sinai Kaskazini wa kaskazini mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Kituo kimoja cha utafiti cha Marekani kimetangaza kuwa, karibu raia 11,000 wa Tunisia walijiunga na magenge ya kigaidi katika nchi za Iraq na Syria.
Wanamgambo kadhaa wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wameangamizwa katika shambulio la anga la jeshi la Iraq lililolenga mkusanyiko wa viongozi wa Daesh katika eneo la al Susah mkoani Deir Zor nchini Syria.
Vikosi vya ulinzi vya Iraq vimetangaza habari ya kusambaratishwa timu nyingine ya magaidi huko magharibi mwa mji wa al Ramadi, makao makuuu ya mkoa wa al Anbar.
Nchi za Magharibi na baadhi ya tawala za kiimla na vibaraka wao katika eneo la Mashariki ya Kati tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran zimekuwa zikiyaunga mkono na kuyasaidia makundi ya kigaidi kwa shabaha ya kutoa pigo kwa taifa la Iran.
Magaidi wasiopungua 15 wa ISIS wameangamizwa kwenye operesheni ya jeshi la Iraq katika mkoa wa Salahuddin wa kaskazini mwa nchi hiyo.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imetangaza kwamba maafisa wa usalama wa nchi hiyo wamewaua wanachama 13 wa kundi moja la kigaidi katikati ya nchi.
Kundi la kigaidi la Tahrir al Sham limehamishia katika eneo la Jasr al Shughur mkoani Idlib huko Syria shehena ya mada za kemikali zenye gesi za Chlorine na Sarine.
Russia imetangaza kuwa, ina habari za kipelelezi kuhusu njama inayopangwa na magaidi kwa ajili ya kutumia silaha za kemikali katika eneo la Idlib huko kaskazini magharibi mwa Syria.