Magaidi wa Daesh waendelea kuangamizwa kaskazini mwa Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i49673-magaidi_wa_daesh_waendelea_kuangamizwa_kaskazini_mwa_iraq
Magaidi wasiopungua 15 wa ISIS wameangamizwa kwenye operesheni ya jeshi la Iraq katika mkoa wa Salahuddin wa kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 21, 2018 23:51 UTC
  • Magaidi wa Daesh waendelea kuangamizwa kaskazini mwa Iraq

Magaidi wasiopungua 15 wa ISIS wameangamizwa kwenye operesheni ya jeshi la Iraq katika mkoa wa Salahuddin wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Shirika la habari la Tasnim limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mmoja wa wakuu wa genge la kigaidi ametiwa mbaroni na askari usalama wa Iraq katika mkoa wa Kirkuk.

Saad Maan, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, kitengo cha operesheni na mapambano dhidi ya ugaidi cha mkoani Kirkuk kimemtia mbaroni kiongozi mmoja wa genge la kigaidi la Daesh ambaye ni maarufu kwa jina la nduli wa Daesh ametiwa mbaroni.

Magaidi wa Daesh wakifanya jinai ya kutisha ya kuwapiga risasi na kuwaua kwa umati raia wa Iraq. Inaonekana haikuwapitikia kabisa akilini mwao kwamba baadaye wangelisambaratishwa vibaya na kuwindwa kama wanyamapori

 

Komandi ya operesheni ya pamoja ya Iraq hivi karibuni ilitangaza habari ya kuanza operesheni kubwa ya askari wa Iraq kwa ajili ya kuwasaka mabaki ya magaidi wa Daesh katika jangwa la magharibi la nchi hiyo.  

Taarifa zinasema pia kuwa ndege za kivita za Iraq zimefanya shambulizi dhidi ya ngome za magaidi hao ndani ya ardhi ya nchi jirani ya Syria.

Hadi hivi sasa askari wa Iraq wamefanikiwa kugundua na kuangamiza makumi ya magaidi wa Daesh waliokwa wamejificha katika maeneo tofauti hasa ya kaskazini mwa nchi hiyo.