-
Umoja wa Mataifa watoa onyo kali kuhusu kuongezeka majanga katika Ukanda wa Gaza
Jun 20, 2024 22:44Francesca Albanese, Ripota wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina, amesema katika taarifa kwamba hali ya maafa huko Ukanda wa Gaza imezidi kuwa mbaya. Kwa kauli yake, utawala haramu wa Israel unalenga misafara ya misaada ya kibinadamu inayotumwa Gaza na kuzuia ufikaji wa misaada katika ukanda huo.
-
Kushambulia Rafah; kipaumbele cha Israeli na kupuuzwa matakwa ya kimataifa
May 30, 2024 23:07Huku ukiwa umepuuza matakwa na maonyo ya kimataifa kuhusu athari na matokeo hatari ya kibinadamu ya kushambuliwa mji wa mpakani wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza, utawala wa Kizayuni umetuma vikosi vya kivita katika eneo hilo, ambapo vinaua kikatili wakazi wake bila kujali lolote.
-
Baraza la Usalama UN lataka uchunguzi huru kuhusu makaburi ya halaiki huko Gaza
May 11, 2024 23:07Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka, huru na wa kina kuhusu ripoti za kugunduliwa makaburi ya halaiki katika Ukanda wa Gaza, likisisitiza haja ya kuruhusiwa wachunguzi kufikia maeneo hayo na kuwawajibisha wale waliohusika na uhalifu huo.
-
Safari ya Abdollahian Gambia kushiriki mkutano wa OIC wa kujadili changamoto za Waislamu hasa Palestina
May 05, 2024 03:26Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yupo Banjul, mji mkuu wa Gambia kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa 15 wa Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, OIC.
-
Kashfa ya kutoweka raia 10,000 wa Palestina katika vita vya Gaza
May 03, 2024 23:00Sambamba na kuendelea kupanuka maandamano ya wanafunzi wa Marekani na juhudi za Mahakama ya ICJ na ICC za kutoa waranti wa kukamatwa viongozi wa utawala wa kibaguzi wa Israel kutokana na jinai zao huko Gaza, Shirika la Haki za Binadamu la Euro-Mediterranean limetoa ripoti mpya na ya kutisha inayoweza kuzidisha hasira za wanafunzi hao na wakati huo huo kuongeza ushahidi mpya katika jinai zinazofanywa na utawala huo dhidi ya Wapalestina.
-
Jitihada za China za kuleta maridhiano ya kitaifa Palestina
May 01, 2024 23:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ametangaza kuwa kufuatia mkutano wa wawakilishi wa harakati za Palestina za Hamas na Fat'h mjini Beijing, pande mbili zimefikia makubaliano ya kujadili maridhiano ya kitaifa huko Palestina.
-
Balozi zote za Israel zawekwa kwenye hali ya tahadhari kuhofia waranti wa ICC wa jinai za vita vya Ghaza
Apr 29, 2024 23:17Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeziagiza balozi zake duniani kote kuwa tayari kwa madhara yanayoweza kutokea iwapo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) itatoa waranti wa kukamatwa maafisa wa utawala huo kwa uhalifu wa kivita na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Uwezekano wa ICC kutoa waranti wa kukamatwa Netanyahu kwa mauaji ya Ghaza umeitia tafrani Israel
Apr 28, 2024 08:15Baraza la mawaziri la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limeingiwa na tafrani na wasi wasi mkubwa juu ya uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa waranti wa kukamatwa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu na maafisa wengine waandamizi kwa kuhusika na jinai za vita vya miezi kadhaa vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza uliozingirwa.
-
UN yaunga mkono maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani ya kuwatetea watu wa Gaza
Apr 28, 2024 00:56Stephen Dujaric Msemaji wa Umoja wa Mataifa jana Ijumaa alisema katika radiamali yake kwa maandamano yanayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu huko Marekani katika kuwaunga mkono watu wa Gaza na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo hilo kwamba: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mfuasi na mungaji mkono mkubwa wa uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na huko Marekani; na anaunga mkono haki ya wananchi ya kufanya maandamano kwa amani.
-
Wachambuzi: Maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani yanamuweka Biden matatani
Apr 27, 2024 08:14Duara la maandamano ya wanafunzi wa vyuo viku dhidi ya vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza linazidi kupanuka nchini Marekani, na kusababisha mkanganyiko mkubwa katika hesabu za Israel na waungaji mkono wake.