Hatimaye utawala wa Kizayuni wakiri kuwa umeua mateka wake Ghaza
(last modified 2024-07-23T06:32:24+00:00 )
Jul 23, 2024 06:32 UTC
  • Hatimaye utawala wa Kizayuni wakiri kuwa umeua mateka wake Ghaza

Baada ya siku 290 za vita, hatimaye jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limekiri kuwa makumi ya mateka wa Kizayuni wameuliwa katika ukanda wa Ghaza na askari wa utawala huo.

Kwa mujibu wa IRNA, Shirika la Redio na Televisheni la Kizayuni limekiri kuhusu kuuliwa makumi ya mateka wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na askari wa utawala huo. Likinukuu jeshi la Kizayuni, shirika hilo limesema: "mateka wawili Waisrael Alex Datsnig na Yugav Bukhstav waliuawa huko Ghaza Disemba iliyopita". 
 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, habari za kuuawa makumi ya mateka wa Kizayuni huko Ghaza na askari wa utawala wa Kizayuni zimekuwa zikichujwa na kudhibitiwa vikali kwa muda wote huu na kuzuiwa kutangazwa.
 
Kuhusiana na suala hilo Shirika la Redio na Televisheni la Kizayuni limetangaza kuwa: mateka 46 kati ya 120 waliosalia huko Ghaza wameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Kizayuni.

Kabla ya hapo, Brigedi za Izzuddin Al-Qassam tawi la kijeshi la harakati ya Hamas zilitoa taarifa kuzihutubu familia za mateka wa Kizayuni ya kwamba: "jeshi lenu linakudanganyeni na linaendelea kukudanganyeni; na kitu pekee linachotaka ni kuwarejesha mateka wakiwa kwenye jeneza".

Image Caption

Mnamo Oktoba 7, 2023, Muqawama wa Palestina huko Ghaza ulijipenyeza kwenye vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyopakana na Ukanda wa Ghaza kupitia operesheni ya kushtukiza na kuwakamata Wazayuni wapatao 250.

 
Baadhi ya mateka hao waliachiliwa huru katika hatua ya kibinadamu iliuyochukuliwa na Muqawama wa Palestina. Idadi nyingine kati yao iliachiliwa huru wakati wa mchakato wa kubadilishana mateka kati ya utawala wa Kizayuni na Hamas. 
 
Wakati karibu miezi tisa imepita tangu ilipotekelezwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na kukamatwa mateka Wazayuni kadhaa na Muqawama wa Palestina, licha ya uvamizi na jinai kubwa zilizofanywa huko Ghaza, utawala wa Kizayuni hadi sasa haujaweza kuwakomboa mateka hao. Idadi kubwa kati yao wameuawa katika mashambulizi ya angani na ya makombora ya mizinga yaliyofanywa na jeshi la Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ghaza.../

 

Tags