-
Iran: Hatima ileile ya kutoroka Afghanistan itawafika askari wa Marekani waliopiga kambi Iraq na Syria
Nov 30, 2023 03:47Mshauri wa ngazi ya juu wa kijeshi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amepongeza Kambi ya Muqawama katika eneo na kusema "kutoroka" ndio hatima ya mwisho itakayovifika vikosi vamizi vya jeshi la Marekani nchini Syria na Iraq kama ilivyotokea Afghanistan.
-
Iran yazionya Marekani na Israel juu ya 'matokeo hasi makali' endapo jinai za kivita zitaendelea Gaza
Nov 28, 2023 09:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amezionya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba zitakabiliwa na "matokeo hasi makali" iwapo zitashindwa kukomesha kikamilifu uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Gaza uliofanywa wakati wa vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya eneo Palestina lililowekewa mzingiro.
-
Baqeri: Manowari ya Deylaman kudhamini usalama kaskazini mwa Iran
Nov 27, 2023 08:57Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kujiunga manowari mpya ya Deylaman kwenye orodha ya meli za kivita za Iran kutaimarisha usalama katika Bahari ya Caspian, kaskazini mwa nchi.
-
Iran: Wapalestina wataamua hatima yao wenyewe
Nov 27, 2023 07:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema taifa la Palestina halitaruhusu ama utawala wa Kizayuni au Marekani kufikia malengo yao haramu, na kusisitiza kuwa hatima ya Palestina ipo mikononi mwa Wapalestina wenyewe.
-
Amir Abdollahian nchini Lebanon; safari yenye malengo kadhaa
Nov 25, 2023 02:54Hossein Amirabdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametembelea Beirut, mji mkuu wa Lebanon ikiwa ni katika muendelezo wa mashauriano yake na viongozi wa eneo kuhusu hujuma ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza ambapo amekukutana na kuzungumza na maafisa wa nchi hiyo pamoja na viongozi wa mrengo wa muqawama wa Lebanon na Palestina.
-
Tume ya Haki za Binadamu ya Iran: Utawala wa Kizayuni hautakwepa kesi mahakama ya ICC
Nov 25, 2023 01:04Katibu wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Idara ya Mahakama ya Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu inalipa mazingatio maalumu suala la kuhakikisha utawala wa Kizayuni wa Israel haukwepi kesi ya kutenda uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
-
Kan'ani: Usitishaji vita Gaza ni hatua ya kwanza ya kusitisha jinai za kivita za utawala wa Kizayuni
Nov 24, 2023 02:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa usitishaji vita wa muda wa kibinadamu uliofikiwa Ukanda wa Gaza ni hatua ya awali kuelekea kusitisha jinai za kivita za utawala wa Kizayuni unaouwa watoto.
-
Raisi: Israel haijaambulia chochote katika vita vyake Gaza
Nov 23, 2023 04:05Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema Israel imefeli kufikia malengo yake yote katika hujuma na mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Eslami: IAEA iache kuingiza siasa kwenye kesi ya Iran
Nov 22, 2023 23:37Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) ameutaka Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ujiepushe na tabia ya kuingiza siasa kwenye faili la nyuklia la Jamhuri ya Kiislamu.
-
Brigedia Jenerali Qaani: Israel ni dhaifu kuliko utando wa buibui
Nov 18, 2023 00:20Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imefichua kuwa utawala haramu wa Israel ni dhaifu kuliko hata nyumba ya buibui.