-
Abdollahian: Jitihada za kusitisha vita Gaza kwa njia za kisiasa zinaendelea
Nov 01, 2023 23:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu na Qatar zinaendeleza juhudi za kisiasa za kutaka kusimamishwa vita kwa muda katika Ukanda wa Gaza haraka iwezekanavyo, huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendelea kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika eneo hilo lililozingirwa.
-
Abdollahian na Haniya wakutana Doha na kujadili matukio ya Ukanda wa Gaza
Nov 01, 2023 01:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, ambapo wamebadilishana mawazo kuhusu matukio yanayoendelea kushuhudiwa katika Ukanda wa Gaza.
-
Jenerali wa Iran: Makamanda wa US wapo Tel Aviv kuongoza mauaji ya kimbari Gaza
Oct 31, 2023 23:32Kamanda wa Kamandi Kuu ya Khatam al-Anbiya ya Jeshi la Iran amesema makamanda wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani katika eneo la Asia Magharibi (CENTCOM), na vile vile makamanda wa Kikosi cha Majini cha nchi hiyo wapo Tel Aviv kuwasaidia maafisa wa utawala haramu wa Israel kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Raisi: Kulaaniwa Israel katika Baraza Kuu la UN ni mafanikio muhimu
Oct 29, 2023 23:30Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya hivi karibuni ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupasisha azimio juu ya vita vya Gaza ni mafanikio muhimu katika mkondo wa kusitisha jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.
-
Diplomasia yenye nguvu na amilifu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Ghaza; tokea safari za kieneo hadi New York
Oct 28, 2023 04:25Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika kuendelea na siasa za diplomasia amilifu na imara kuhusu Ghaza, amesafiri mjini New York ambapo ameshiriki katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza juu ya haja ya kuchukuliwa hatua muhimu za dharura ili kukomesha vita huko Ghaza
-
Amir Abdollahian: Utawala wa Kizayuni unafanya mauaji ya kimbari huko Gaza
Oct 27, 2023 02:21Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya mauaji ya kimbari huko Gaza.
-
Kubainishwa misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na vita vya Gaza
Oct 25, 2023 04:19Siku 19 zimepita tangu kilipoanza Kimbunga cha Al-Aqsa na vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. Suali muhimu la kujiuliza hapa ni je, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa na msimamo gani kuhusiana na vita hivi na imechukua hatua gani?
-
Iran: Marekani ni mshirika wa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza
Oct 25, 2023 04:07Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Marekani ni mshirika katika jinai za kutisha za Israel huko Ukanda wa Gazal kutokana na uungaji mkono wake usio na kifani kwa utawala huo unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Waziri wa Ulinzi: Maadui wanaogopa jibu kali la Iran
Oct 24, 2023 23:22Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema hatua yoyote ghalati ya maadui itaipelekea Jamhuri ya Kiislamu itoe jibu kali na la kuumiza, na ambalo litamfanya adui ajutie.
-
"Shambulio la Israel dhidi ya kanisa Gaza linakumbusha tabia za ISIS"
Oct 21, 2023 04:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani shambulizi la Israel dhidi ya Kanisa la Saint Porphyrius katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, "Shambulio la Israel dhidi ya kanisa Gaza linashabihiana na nyendo za kundi la kigaidi la ISIS."