-
Kuongezeka kwa kasi biashara ya nje ya Iran katika serikali ya 13 licha ya kuwepo vikwazo vya upande mmoja vya Marekani
Feb 27, 2022 22:51Biashara ya nje ya Iran katika kipindi cha miezi 11 iliyopita imefikia kiwango cha dola bilioni 90, ambalo ni ongezeko la asilimia 38 ikilinganishwa na muda kama huo katika mwaka uliopita.
-
Amir-Abdollahian: Mazungumzo ya Vienna yatafanikiwa iwapo nchi za Magharibi zaitabadilisha msimamo
Feb 27, 2022 01:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefanya mazungumzo ya simu na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na kusema baadhi ya masuala muhimu yaliyosalia katika mazungumzo ya Vienna ya kuondolewa Iran vikwazo yanaweza kutatuliwa.
-
Mazungumzo ya simu ya Marais wa Iran na Russia
Feb 27, 2022 00:22Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Ebrahim Raisi, na Rais wa Russia, Vladimir Putin, walifanya mazungumza ya simu Alhamisi iliyopita kuhusu masuala ya kimataifa na mazungumzo yanayoendelea huko Vienna kuhusu suala la kuondolewa vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Iran.
-
Iran kuendelea kurutubisha urani kwa 20% hata ikiondolewa vikwazo
Feb 25, 2022 23:09Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuzalisha madini ya urani iliyoritubishwa kwa kiwango cha asilimia 20, hata kama itaondolewa vikwazo katika mazungumzo ya Vienna yanayolenga kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Mauzo ya mafuta ya Iran nje ya nchi yaongezeka kwa 40%
Feb 25, 2022 23:08Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema uuzaji wa mafuta yake katika soko la kimataifa umeongezeka kwa asilimia 40 katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, licha ya vikwazo dhidi ya taifa hili.
-
Iran yapinga kutumiwa haki za binadamu kama chombo dhidi ya nchi zingine
Feb 24, 2022 23:48Katibu wa Baraza la Haki za Binadamu la Iran amekutana na mabalozi wa Russia na China nchini Iran ambapo wametangaza kwa pamoja kupinga kutumiwa vibaya kadhia ya haki za binadamu kama chombo cha kuyashinikiza mataifa mengine.
-
Gesi asilia; jibu kwa changamoto za ustawi endelevu katika karne ya 21
Feb 23, 2022 08:17Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi Zinazouza Nje Gesi Asilia (GECF) ulianza rasmi Jumanne wiki hii ukihudhuriwa na Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wakuu na wawakilishi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Mkutano huo ilifunguliwa kwa hotuba ya Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani kwa kauli mbiu ya "Usalama wa Nishati Duniani".
-
Iran: Tuko tayari kustawisha uhusiano wetu na nchi za Afrika katika nyuga tofauti
Feb 23, 2022 03:43Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kuimarisha na kustawisha uhusiano wake katika nyuga mbalimbali na nchi za Afrika kama vile kupeleka barani humo uzoefu wake wa kiufundi na kihandisi.
-
Raisi atoa mwito wa kustawishwa uhusiano wa Iran na Msumbiji
Feb 22, 2022 23:21Rais Ebrahim Raisi wa Iran ametoa mwito wa kuboreshwa uhusiano wa pande mbili baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Msumbiji katika nyuga tofauti.
-
Iran: Uingiliaji wa US, NATO umeshadidisha mgogoro wa Ukraine
Feb 22, 2022 23:12Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa vikali chokochoko za Marekani na shirika la kijeshi la NATO katika mgogoro wa Ukraine na kusisitiza kuwa, uingiliaji huo umeshadidisha taharuki mashariki mwa nchi hiyo jirani na Russia.