-
Iran: Hakuna mazungumo yanayohitajika kwa Marekani kurejea katika JCPOA
Mar 11, 2021 23:11Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema mpango wa Marekani wa kutaka kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hauhitaji mazungumzo yoyote kwani Washington haikufanya mazungumzo wala mashauriano na yeyote wakati wa kujiondoa katika mapatano hayo ya kimataifa.
-
Rouhani: Wazayuni wanataka vikwazo dhidi ya Iran viendelee
Mar 10, 2021 08:37Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Wazayuni na watawala wasiotaka mageuzi katika eneo wanataka vikwazo vya kidhalimu dhidi ya watu wa Iran viendelee.
-
Rais Rouhani: Njia pekee bora ya kuyakurubisha pamoja mataifa ya dunia ni kujiimarisha kielimu na kiutamaduni
Mar 09, 2021 23:19Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia pekee ya kudumu kwa ajili ya kuyafanya mataifa ya dunia yakurubiane zaidi, ni kujiimarisha kielimu na kiutamaduni.
-
Meja Jenerali Safavi: Iran iko katika kilele cha uwezo wa kujihami angani
Mar 07, 2021 23:13Mshauri wa Ngazi za Juu wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Iran hivi sasa iko katika kilele cha uwezo wa kujihami hasa katika uga wa angani.
-
Iran kujenga bandari kubwa zaidi ya kibiashara katika Bahari ya Oman
Mar 07, 2021 04:31Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Bandari na Ubaharia la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza habari ya kujengwa bandari kubwa zaidi ya kibiashara ya Iran katika Bahari ya Oman na katika eneo la Kuhe Mubarak katika wilaya ya Jask katika mkoa wa Hormozgan, kusini mwa nchi.
-
Rouhani: Iran inalipa kipaumbele suala la Usalama na amani Iraq
Mar 07, 2021 01:17Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi na kusisitiza kuwa, usalama, mshikamano na amani Iraq ni kipaumbele muhimu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Jibu la Zarif kwa Sherman; mazungumzo mapya kuhusu mapatano ya JCPOA ni marufuku
Mar 06, 2021 22:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena amesema kuwa mapatano ya JCPOA hayawezi kujadiliwa upya. Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo akijibu ombi la serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani la kutaka mazungumza mapya yafanyike kuhusu suala hilo.
-
Arab League yatakiwa iache kutoa taarifa zisizo na msingi
Mar 06, 2021 04:47Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaka Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ijiepushe na tabia yake ya kutoa taarifa zisizo na msingi wowote na badala yake, ikumbatie mambo ambayo yanaweza kuimarisha ushirikiano wa nchi za eneo.
-
Iran yaionya Israel dhidi ya kuchukua hatua yoyote ghalati
Mar 06, 2021 04:44Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kuchukua hatua yoyote ghalati kwa kisingizio cha mripuko uliotokea katika meli ya utawala huo katika Bahari ya Oman wiki iliyopita.
-
HAMAS: Tuna uhusiano mzuri sana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Mar 05, 2021 23:25Osama Hamdan, mjumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, harakati hiyo ina uhusiano mzuri na imara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.