Meja Jenerali Safavi: Iran iko katika kilele cha uwezo wa kujihami angani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i67634-meja_jenerali_safavi_iran_iko_katika_kilele_cha_uwezo_wa_kujihami_angani
Mshauri wa Ngazi za Juu wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Iran hivi sasa iko katika kilele cha uwezo wa kujihami hasa katika uga wa angani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 07, 2021 23:13 UTC
  • Meja Jenerali Safavi: Iran iko katika kilele cha uwezo wa kujihami angani

Mshauri wa Ngazi za Juu wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Iran hivi sasa iko katika kilele cha uwezo wa kujihami hasa katika uga wa angani.

Meja Jenerali Sayyid Rahim Safavi, Mshauri wa Ngazi za Juu wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo Jumapili alipohutubia hadhara ya wahadhiri na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Anga cha Ashura mjini Tehran na kuongeza kuwa: "Adhama ya uwezo wa sasa wa Jeshi la Anga la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu haiwezi kulinganishwa na zama za Kujihami Kutakatifu."

Mshauri wa Ngazi za Juu wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa,  dunia ya sasa inabadilika kwa kasi kubwa sana na mabadiliko hayo yanashuhudiwa zaidi katika bara Asia hasa Asia Magharibi. Amesema katika kipindi cha miaka 30 ijayo,  hakutakuwa na nchi yoyote itakayotambulika kama dola pekee lenye nguvu zaidi duniani kwani hivi sasa dunia inaelekea katika upande wa kuwepo madola kadhaa yenye nguvu.

Kombora la Emad ambalo limeundwa kikamilifu nchini Iran likifanyiwa majaribio

Aidha amesema sababu iliyopelekea Marekani ihasimiane na Iran haina uhusiano na kadhia ya nyuklia au makombora bali sababu kuu ni kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanapingana na fikra ya mfumo wa kibeberu duniani.

Aidha amesema Wamarekani na Wazayuni wameingiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na nguvu na uwezo wa taifa la Iran, Kiongozi Muadhamu na Mapinduzi ya Kiislamu katika eneo la Asia Magharibi. Amesema mapambano ya taifa la Iran na uongozi imara wa Kiongozi Muadhamu ni mambo ambayo yamepelekea njama za maadui kusambaratika.