-
Iran: Vikwazo vipya vinaashiria namna Marekani isivyoheshimu sheria za kimataifa
Jun 25, 2019 03:19Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ni ithibati nyingine tosha kuwa utawala wa Washington hauko tayari kuheshimu sheria za kimataifa.
-
Wasiwasi wa Uingereza kuhusu uwezekano wa kutokea 'vita vya ghafla' kati ya Iran na Marekani
Jun 24, 2019 23:07Serikali ya London haidhani kwamba Tehran na Washington zinataka vita lakini ina wasiwasi mkubwa kuhusiana na uwezekano wa kutokea 'vita vya ghalfa' kati ya Iran na Marekani.
-
Zarif: Vikwazo vya Marekani vinalemaza vita dhidi ya mihadarati
Jun 24, 2019 08:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo vya upande mmoja vya Marekani na ugaidi wa kiuchumi wa nchi hiyo ya kibeberu dhidi ya taifa la Iran umekuwa kizingiti kikubwa katika ushirikiano wa kimataifa hususan katika vita dhidi ya mihadarati.
-
Zarif: Timu B ilijaribu kumtia mtegoni Trump aingie katika vita na Iran
Jun 23, 2019 23:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema tukio la hivi karibuni la drone ya Marekani kukiuka anga ya Iran katika Bahari ya Oman ilikuwa sehemu ya njama pana za wapenda vita (Timu B) kumtia mtegoni Rais Donald Trump wa Marekani ili aingie katika vita na Iran.
-
Sanders: Trump amelazimika kuzima moto aliouwasha dhidi ya Iran
Jun 23, 2019 22:30Seneta Bernie Sanders ambaye ametangaza azma yake ya kugombea tena urais katika uchaguzi wa urais nchini Marekani mwaka ujao amesema Rais Donald Trump wa nchi hiyo amelazimika kuzima moto wa mgogoro na taharuki aliouwasha mwenyewe dhidi ya Iran.
-
Pentagon: Marekani haitaki kuingia vitani na Iran
Jun 22, 2019 23:01Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imesema kuwa, nchi hiyo haina nia ya kuingia vitani na Iran, lakini imedai kwamba italinda maslahi yake katika eneo.
-
Saudia iliiomba Uingereza iishambulie kijeshi Iran, baada ya Marekani kukwepa kufanya hivyo
Jun 22, 2019 08:34Mkuu wa Idara ya Ujasusi wa Saudi Arabia aliiomba serikali ya Uingereza ishambulie kambi na vituo vya kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, masaa machache baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kuwa amesitisha kile alichokitaja kama shambulizi la ulipizaji kisasi la Washington dhidi ya Tehran.
-
Russia yalaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
Jun 22, 2019 08:16Vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Iran ni vikwazo vilivyo kinyume cha sheria na vinavyokinzana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. Nchi za kundi la 4+1 limelaani vikwazo hivyo dhidi ya Iran.
-
Iran: Hatukaribishi vita lakini tuko tayari kujihami kwa nguvu zote
Jun 22, 2019 07:40Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesema kuwa, majeshi na wananchi wa Iran hawataki vita lakini daima wako imara kuihami na kuilinda nchi yao.
-
UN haijaafiki madai ya Marekani kuhusu drone yake iliyoangushwa na Iran
Jun 22, 2019 03:20Umoja wa Mataifa umejibu madai ya wakuu wa Marekani kuwa drone yao ya kijasusi iliyoangushwa na Iran iliangushwa katika maji ya kimataifa katika Ghuba ya Uajemi.